TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, March 31, 2015

Ubunifu mwingine kwenye mijengo mtu wangu.. Nimevutiwa sana na hizi PICHAZ

. 
Maajabu ya kuvutia.. yani zimetengenezwa nyumba na Hotel kwa ubunifu wa nguvu mtu wangu.
Nyumba za vioo, nyumba za miti.. Ziko nyingi hapa mtu wangu, unaweza kuzicheki zote.
.
Free Spirit Spheres, Canada. Utalii mwingine mzuri ndani ya nchi hiyo.
.
Boat Hotel. Hii Hotel vyumba vyake viko kama boti hivi, iko Visiwa vya Maldives, Asia.
La-Balade-Des-Gnomes-669x445
Trojan Horse Hotel. Kwa haraka haraka unaweza usijue hiki ni nini, lakini unaambiwa hii ni Hotel, hapo ndani kuna vyumba vya kulala na kila kitu kinaenda poa kabisa.
.
Ark Hotel, China. Wachina na teknolojia zao mtu wangu, hii Hotel imetengenezwa kwenye maji inaelea yani. Hapo unaweza kuona kwa juu inavyoonekana na kwa ndani ya maji pia.
.
Mirror Tree House, Sweden. Hapo panapoonekana kama mwanga mwekundu ni chumba cha Hotel yani, kimejengwa kwa vioo vitupu. Utakuwa na amani kweli kulala hapo?
.
Castle Hotel, Austria. Yani ni kama unauangalia Mlima hivi, karibu sana Austria mtu wangu.
.
Unadhani hii ni karavati ya barabarani? Hapana.. Ni vyumba vya Das Park Hotel, iko Austria. Vyumba nd’o viko hivyo yani. Mambo ya Ulaya Ulaya.
.
Umeielewa hii? Ni Hotel inayoitwa Airplane, iko Costa Rica. Hapo vipi mtu wangu, umevutiwa na hii?
attrap_reves_bubble_hotel
Bubble Hotel, unaweza kujionea hiii mtu wangu ukitembelea Ufaransa. Moja ya story zilizosikika March 2015 ni malalamiko ya baadhi ya watu kwamba hakuna usiri wowote ukiwa ndani ya chumba hicho cha Hotel.
.
Utajisikiaje kuwa kwenye hiki chumba cha kioo? Aina hii ya kioo ni kama kile kioo cha kujiangalizia.. mtu aliye nje haoni ndani. Hiki ni chumba cha Mirror Hotel, Berlin Ujerumani.
.
Hotel hii iko chini ya maji visiwa vya Fiji mtu wangu.
montana-magica-lodge_13
Magic Mountain Hotel, hii iko Panguipulli, Chile. Ukiiangalia kwa haraka ni kama Mlima uliozunguka na vichaka, hiyo ni Hotel mtu wangu.

No comments:

Post a Comment