MT. MERU YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MASHUKA KUJIFUNIKIA WAGONJWA
Hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mashuka ya kujifunikia kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali waliolazwa hospitalini hapo hali ambayo imepelekea baadhi ya wagonjwa hao kulala bila kujifunika nyakati za usiku.
Kwa sasa hospitali hiyo ina jumla ya vitanda 500 na mashuka 300 wakati wastani wa kitanda kimoja kinatakiwa kuwa na mashuka 8.
Akizungumza
na waaandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada wa jumla ya
mashuka 100 na katoni kumi za maji kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa
hospitalini hapo,muuguzi mfawidhi wa hospitali hiyo,Sifael Masawe
alisema kuwa tatizo la uhaba wa fedha kutoka serikali kuu limechangia
kukosekana kwa huduma mbalimbali hospitalini hapo yakiwemo mashuka.
Alisema
kuwa kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa hushindwa kujifunika mashuka
nyakati za usiku kutokana na uhaba wa mashuka hayo na kuwataka wadau
mbalimbali mkoani Arusha kujitokeza kuokoa hali hiyo.
Akikabidhi
misaada ya mashuka na maji kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika wodi
wa akina mama hospitalini hapo ,mwenyekiti wa kikundi cha Upendo
Family,Faustine Mwandago alisema kwamba misaada hiyo imegharimu kiasi
cha zaidi ya sh,2 milioni.
Mwandago,alisema
kuwa lengo la kukabidhi misaada hiyo ni kuonyesha upendo kwa watu wenye
mahitaji mbalimbali sanjari na kulienzi jina la kikundi chao kwa
vitendo huku akiwataka wadau wengine kuwaunga mkono.
No comments:
Post a Comment