TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, March 6, 2015

Kwenye zile kali za mwaka !!! hii ya Wanaume 400 kukata uume wao uliipata?

Saint_Gurmeet_Ram_Rahim_Singh_Ji_Insan 
Ishu ya imani ni ya mtu binafsi na kila mtu anauwezo wa kuamini kile anachoona ni sahihi kwa mtazamo wake na mtu anapotokea kumuamini kiongozi wake wa dini kwa asilimia kubwa hutekeleza yale aliyofundishwa.
Sasa hii ya leo inamuhusu muhubiri  maarufu wa dini nchini India ambae anawafuasi milioni hamsini duniani  Gurmeet Ram Rahim Singh anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha majeruhi kwa tuhuma za kufanikiwa kuwashawishi wafuasi wake wapatao 400,  kukata sehemu zao za siri ili waweze kuwa karibu na Mungu.
MSG-The-Messenger-of-God-Movie-Critics-Reviews-Public-Reviews-Ft.-Gurmeet-Ram-Rahim-Singh 
Wafuasi wa Singh walikata sehemu zao za siri kwenye Hospitali ambayo yeye ndio mmiliki ambapo kwenye headlines nyingine muhubiri huyu amekuwa akihusishwa na mauaji ya mwandishi wa habari za uchunguzi pamoja na kutuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia lakini hajawahi kushtakiwa.
Mmoja wa wafuasi wake Hans Raj Chauhan aliwaambia Polisi kwamba alikatwa sehemu zake za siri kwa sababu alidhani asingetakiwa kwenye jamii kama angekataa kutekeleza hilo jambo lililoanzishwa na Singh.
Singh aliwaambia wafuasi wake kwamba wale ambao wafatekeleza amri hiyo watakuwa na uwezo wa kumuona Mungu.

No comments:

Post a Comment