Watu watatu wauawa katika shambulio dhidi ya Minusma Kidal
Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakipiga doria katika mji wa Kidal, mwezi Julai mwaka 2013.
Na RFI
" Kambi
ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma),
imeshambuliwa Jumapili Machi 8 kwa makombora zaidi ya thelathini",
kikosi cha Umoja wa mataifa nchini Mali kimetangaza katika tangazo
kiliyotoa Jumapil hii.
Hata
hivyo kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali kimebaini kwamba kimeweza
kujibu shambulio hilo. Shambulio ambalo limegharimu maisha ya watu
watatu ikiwa ni pamoja na mwanajeshi mmoja wa kikosi cha Umoja wa
Mataifa na raia wawili wa kawaida, huku zaidi ya watu 20 ikiwa ni pamoja
na wanajeshi wanane wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakijeruhiwa.(P.T)
Shambulio hilo linatokea siku moja kabla ya kutokea kwa machafuko katika mji wa Gao.
Shambulio
la kwanza lilitokea mapema asubuhi kabla ya kuzimwa na wanajeshi wa
kikosi cha Umoja wa Mataifa. Lakini muda mchache baadae, shambulio
jingine limetokea katika eneo kunakopatikana kambi ya kikosi cha
wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi
wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, ambao ni washirika wa kikosi cha
wanajeshi wa Ufaransa Barkhane katika eneo hilo wamejibu shambulio na
kufanikiwa kulizima.
Katika
hali ya kubadilishana risasi, baadhi ya makombora yaliangukia katika
eneo linalokaliwa na raia, karibu kilomita tatu na kambi hiyo ya kikosi
cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa katika mji wa Kidal, na kupelekea
watoto wawili kufariki. Upande wa Minusma mwanajeshi mmoja kutoka Chad
ameuawa.
Hali hii
imezua mvutano mkubwa baina ya viongozi na raia, ambapo maswali yamekosa
majibu. Baadhi wanajiuliza iwapo makombora hayo yaliyorushwa hadi
katika eneo linalikaliwa na raia yametokea katika kambi ya kikosi cha
wanajeshi wa Umoja wa Mataifa, huku wengine wakijiuliza iwapo makombora
hayo yalitokea upande wa kambi ya wanamgambo wa kiislamu.
Kundi la
wanajihadi linaloendesha harakati zake nchini Algeria Mali Mokhtar
Belmokhtar, linadaiwa kuwa ndilo limetekeleza mashambulizi hayo dhidi ya
kambi ya wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali.
Umoja wa
Mataifa umelani mashambulizi hayo dhidi ya kambi ya wanajeshi wake.
Mashambulizi ambayo yamegharimu maisaha ya watu watatu, ikiwa ni pamoja
na mwanajeshi mmoja wa kikosi hicho kutoka Chad pamoja na watoto wawili.
No comments:
Post a Comment