Kenya:Mwili wa shahidi aliyeuawa wapatikana
Uchunguzi wa chembechembe za DNA umehakikisha kuwa ni mwili wa shahidi wa mahakama ya ICC
Serikali
ya Kenya imeutambua rasmi mwili wa jamaa mmoja uliopatikana katika mbuga
ya wanyama, kuwa ni wa shahidi wa mahakama ya ICC, Meshack Yebei,
katika kesi inayomkabili makamu wa rais wa Kenya, William Ruto.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, uchunguzi wa chembechembe za DNA umehakikisha fika kuwa ni yeye.
Tangazo
hilo linatarajiwa kuipa afueni familia ya Yebei, ambayo nusura izike
mwili tofauti mnamo mwezi Januari, kabla ya kuambia kwamba mwili huo
haukuwa wa mtoto wao.
Mwanachemia
wa serikali ya Kenya hatimaye ametangaza kuwa mwili Fulani ambao
umelala kwenye chumba cha kuhifadhia maiti tangu mwezi Desemba ni wa
Meshack Yebei.
Bwana
Yebei alitarajiwa kuwa shahidi wa mshtakiwa kwenye kesi dhidi ya Makamu
wa Rais wa Kenya, William Ruto, anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji
katika mahakama hiyo ya kimataifa huko Hague.
Gazeti
moja la Kenya limemnukuu afisa wa uchunguzi akisema kwamba chembechembe
za DNA zimedhibitisha kwamba mwili huo uliopatikana ni wa Yebei.BBC
ICC imefichua kuwa marehemu alipewa nafasi ya kupata ulinzi na makazi salama lakini akakataa
Matokeo haya ni sambamba na yale yaliyochapishwa na daktari mmoja wa Afrika Kusini aliyepewa kazi hiyo na familia.
Inatarajiwa kuwa serikali sasa itafanya uchunguzi wa pili kugundua kilichosababisha kifo chake.
Inasemekana
kwamba Meshack Yebei alitekwa nyara mwishoni mwa mwezi Desemba nyumbani
kwake Eldoret alipokwenda kumwona mkewe ambaye alikuwa anaugua.
ICC imefichua kuwa marehemu alipewa nafasi ya kupata ulinzi na makazi salama lakini akakataa.
Mwezi
Januari mwili ulioharibika vibaya ulipatikana katika mto ulio takriban
kilomita arobaini kutoka nyumbani kwake, na familia ikadhani kuwa ni
yeye.
ICC imefichua kuwa marehemu alipewa nafasi ya kupata ulinzi na makazi salama lakini akakataa.
Lakini uchunguzi wa DNA ukaonyesha kuwa ni mwili wa mtu mwengine ambaye pia alitoweka wakati huo huo.
Kufikia
wakati huo familia yake tayari ilikuwa inalalamika kuwa kutoweka kwake
Yebei kunatokana na kuhusishwa na kesi hiyo nyeti.
Ufumbuzi huu sasa unaibua maswali mapya.
Mbuga ya
Wanyama ya Tsavo, ambako mwili huo ulipatikana, iko takriban kilomota
mia sita kusini mashariki mwa Eldoret alikotoweka.
Aidha
familia yake imelalamika kuhusu muda ambao serikali imechukua kutangaza
matokeo ya DNA, na imetishia kuuchukua mwili huo ili iuzike wiki hii,
iwapo serikali itatoa thibitisho hilo au la.
No comments:
Post a Comment