Walimu wa jimbo la uzini wafanya ziara ya kimasomo mkoani Lind
Mke wa
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete amefurahishwa
na hatuwa iliyochukuliwa na Walimu wa Jimbo la Uzini Zanzibar ya
kufanya ziara ya kimasomo Mkoani Lindi kwani ni njia moja wapo ya
kujifunza na kujiongezea elimu kwa vitendo.
Hayo
ameyasema Jana wakati akiwakaribisha walimu wa Jimbo hilo Mkoani hapo
kwa ajili ya kuanza rasmi ziara yao ambayo inatarajiwa
kuchukuwa takribani wiki moja.
Aidha
Mama Salma amesema ziara za kimasomo ni njia moja ya kuleta mashirikiano
na kudumisha Muungano wa Watanzania katika kuboresha Sekta ya Elimu
Nchini hiyo ni kwa sababu Elimu ya Juu na Sekondari nchini Tanzania ni
moja ya mambo yaliyo chini ya Serikali ya Muungano.
Akizungumzia
Changamoto zinazowakabili Walimu hao katika Sekta ya Elimu kwa upande
wa Mkoa wa Lindi ni upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi jambo ambalo
husababisha kukosekana kwa wataalamu wa fani mbalimbali za Kisayansi
kwa maendeleo ya Taifa ambapo hurudisha nyuma jitihada zao za kutaka
kuzalisha wataalamu watakaokwenda sambamba na ulimwengu wa Sayansi na
Teknolojia.
Nae Afisa
Uendeshaji wa Wizara ya Elimu Zanzibar Nd. Muhussin Sufiani Mkanga
amesema lengo kuu la ziara hiyo ni kujifunza njia mbalimbali zilizobora
za kielimu ikiwa ni njia za kuwafundishia wanafuzi wa Zanzibar katika
kuimarisha ufaulu mzuri kwa wanafunzi wa Kidato cha Nne.
Hata
hivyo amewataka walimu wenzake waliopata fursa kuwepo katika ziara hiyo
kuwa makini katika kujifunza masomo hayo kwa lengo la kupata njia zilizo
bora za utoaji wa elimu kwa wanafunzi wao ikiwa ni mfano mzuri wa
kuigwa na walimu wengine Nchini.
Jumla ya
walimu 36 kutoa Zanzibar wamepata fursa ya ziara ya kimasomo Mkoani
Lindi na wanatarajiwa kuwa mabalozi wazuri kwa walimu wenzao waliokosa
fursa hiyo kwa kuwapa yale yote mazuri waliyoyapata na kuyafanyia kazi
kwa maendeleo ya Nchi yao.
No comments:
Post a Comment