Hussein Radjabu atoroka jela na baadhi ya askari polisi
Prosper Niyoyankana (picha), mwanasheria wa Hussein Radjabu.
Na RFI
Kiongozi
wa zamani wa chama tawala Cndd-Fdd nchini Burundi, Hussein Radjabu
anasadikiwa kuwa ametoroka jela usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu Machi
2 mwaka 2015. Hussein Radjabu alikua akizuiliwa jela kwa kipindi cha
zaidi ya miaka 7, tangu mwaka 2007.
Hussein
Radjabu alifungwa jela kwa tuhuma za kupanga njama za mapinduzi dhidi ya
utawala wa Pierre Nkurunziza. Alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela.
Wadadisi wanasema kutoroka kwa Hussein Radjabu ni pigo kubwa kwa utawala wa Pierre Nkurunziza.(P.T)
Hata hivyo wafuasi wengi wa kinara huyo wa zamani wa chama tawala Cndd-Fdd, wanahisi kwamba huenda ameondolewa jela na kuuawa.
Kiongozi
wa jela kuu la Mpimba, mjini Bujumbura, ambako amekua akizuiliwa Hussein
Radjabu, amethibitisha taarifa ya kutoroka kwa kinara huyo wa zamani wa
chama tawala.
Lakini
mwanasheria wake, Prosper Niyoyankana ameiomba serikali ya Burundi
kufanya kilio chini ya uwezo wake ili kifahamishe wapi amepelekwa mteja
wake. Prosper Niyoyankana anahisi kwamba mteja wake ameuawa.
Hayo
yanatokea wakati kunaripotiowa mpasuko katika chama tawala, baada ya
baadhi ya wafuasi vigogo wa chama hicho kutoa misimamo yao kuhusu
kugombea kwa rais Pierre Nkurunziza kwa muhula wa tatu.
Rais
Pierre Nkurunziza anakabiliwa na upinzani ndani na nje ya chama chake
hususan vyama vya upinzani, mashirika ya kiraia pamoja na Kanisa
Katoliki nchini Burundi.
Hayo
yanajiri wakati serikali ya Burundi iliandaa mwishoni mwa juma
lililopita maandamano ya amani ambayo yaliitikiwa na halaiki ya watu,
wengi wao wakiwa wanafunzi na wafanyakazi wa serikali.
Upinzani
ulidai kwamba maandamano hayo yaliandaliwa na chama tawala ili kuonesha
kuwa kina wafuasi wengi, huku baadhi ya mashirika ya kiraia yakikosoa
maneno yaliyokua yakitumiwa na waandamanaji kama vitisho kwa baadhi ya
viongozi wa mashirika hayo ya kiraia.
No comments:
Post a Comment