Wakazi wa kata ya kidete wilayani kilosa,Morogoro wako hatarini kukubwa na mafuriko na njaa
Wakazi wa
kata ya kidete wilayani kilosa, Morogoro wako hatarini kukumbwa na
mafuriko na baa la njaa kufuatia kingo za bwawa kidete lililojengwa ili
kuzuia maji yanayotiririka kutoka milimani na kuzua maafa ya mara kwa
mara kwenye wilaya hiyo kupasuka na kuharibu maelfu ya hekari za
mashamba huku pia hali hiyo ikitishia usalama wa reli ya kati ambayo ni
kiungo kikubwa cha usafiri wa abiria na mizigo ndani na nje ya nchi.
Hofu ya
kuzuka kwa mafuriko hasa kipindi hiki cha masika inaibuka kwa wakazi wa
kata hiyo baada ya kingo za bwawa la kidete linalodaiwa kutafuna zaidi
ya shilingi bilioni 3.5 kubomoka wakati ujenzi wake ukiendelea hali
inayosababisha maji kutiririka kwa wingi na kuingia katika maeneo ua
makazi na tayari yameshakwisha haribu maelfu ya hekari za mashamba na
endapo mvua zitaendelea kunyesha kwa wingi maji hayo huenda yakaleta
madhara kwenye reli ya kati amabayo inapita wilayani humo.
Mbali na
kuzua hofu ya janga la mafuriko na baa la njaa kutokana na kuvunjika kwa
bwawa hilo ambalo asili yake lilijengwa na wajerumani ili kuzuia maji
yasiharibu miundombinu ya reli lakini pia lilikuwa likitoa ajira ya
uvuvi kwa vijana ambao hapa wanaonyesha masikitiko yao ya kukosa kipato.
ITV
inazungumza na mwenyekiti wa kijiji cha kidete stesheni yusuph bakari
ambaye mradi wa bwawa hilo unatekelezwa katika eneo lake analalamikia
siasa kuingizwa kwenye ujenzi wake ambao tayari umetafuna mabilioni ya
fedha za walipakodi huku kukiwa hakuna dalili zozote za kukamilika kwa
wakati. (CHANZO:ITV)
No comments:
Post a Comment