TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, March 6, 2015

Manny Pacquiao tayari kaingia mtaani kujiandaa na pambano lake na Mayweather (Pichaz)

man2 
Ni pambano ambalo mashabiki wengi wa ngumi duniani wanalisubiri kwa hamu kubwa, kumuona Floyd Mayweather na Manny Pacquiao kwenye pambano litakalofanyika May 2 Las Vegas, Marekani.
Manny Pacquiao ameanza kujiandaa tayari, hataki kushindwa na mpinzani wake mwenye vioja vingi, Floyd Mayweather.
pac
Bondia huyo amekuwa akifanya mazoezi katika mitaa ya jiji la Los Angeles kwa siku ya tatu mfululizo na aliongozana na mbwa wake pamoja na timu yake yote ya ufundi wakati wote wa mazoezi.
man
Baada ya hapo alitoa shoo kwa kupiga ngumi huku na kule kuonyesha kwamba anataka kutoa somo kwa Mayweather ambaye wengi wanampa nafasi kubwa ya kushinda.
man4
Pambano kati ya wakali hawa litakuwa pambano la hela nyingi baada ya kuahidiwa kitita kikubwa cha fedha na pia litakuwa gumu kati ya wawili hao.
sukum

No comments:

Post a Comment