TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, March 18, 2015

Taarifa mpya kuhusu bondia Francis Cheka iko hapa

cheee 
Unakumbuka ile ishu ya bondia wa ngumi Francis Cheka ya kumpiga na kumuumiza meneja wa baa yake akimtuhumu kusababisha hasara?
Taarifa iliyotolewa na kocha wake Abdalah Komando na kuthibitishwa na wanafamilia yake inasema Bondia huyo nyota zaidi nchini sasa ameachiwa huru na atakuwa akitumikia kifungo cha nje.
Alisema Cheka ameachiwa huru baada ya kushinda rufaa yake aliyokata kupinga kifungo cha miaka mitatu gerezani na sasa anatumikia kifungo cha nje.
Tayari Cheka alianza kutumikia kifungo hicho mjini Morogoro lakini taarifa za uhakika zinasema ameachiwa leo baada ya kushinda rufaa hiyo na Mahakama kumbadilishia adhabu.
Tayari ameachiwa, Ila tayari yuko nje, tunashukuru kwa hatua hii lakini bado kesi yake inaendelea kwa kipindi chote cha miaka mitatu”; alisema kocha wake Abdalah Komando.
Cheka alihukumiwa kwenda jela baada ya kumuumiza meneja wa baa yake mjini Morogoro akimtuhumu kumsababishia hasara katika baa yake.

No comments:

Post a Comment