Wabunge zaidi ya 10 watajiunga nami - Zitto
Aliekuwa
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA),Zitto Kabwe akionyesha kadi ya Chama chake kipya
yenye namba 007184 mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano
wa Chama cha ACT-Tanzania,uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya
Serena,jijini Dar es Salaam
Akizungumza
na gazeti la HabariLeo jana jijini Dar es Salaam, baada ya kuzungumza
na waandishi wa habari, aLIYEKUWA Mbunge wa Kaskazini, Zitto Kabwe
aliyejiunga rasmi na chama cha siasa cha ACT alisema nyuma yake wapo
wabunge zaidi ya 10, watakaojiunga na ACT muda sio mrefu.(P.T)
"Siko
mwenyewe wapo wenye mapenzi mema na tunataka kufungua ukurasa mpya kwa
nchi yetu wa siasa za kujenga nchi, wabunge mahiri wa CCM na Chadema
zaidi ya 10, watajiunga nami, ila sitakutajia majina kwa sasa kwa sababu
ya sheria za vyama vyao, acha wamalizie vipindi vyao vya ubunge,"
alisema Zitto.
Zitto alisema amelipia ada ya miaka kumi ya uanachama wa chama hicho, ambayo kila mwaka ada ni Sh 1,000.
"Nimejiunga
rasmi na ACT na nimelipa ada ya miaka 10 ya uanachama, nawakaribisha
wote wenye mapenzi mema ya kujenga nchi wajiunge nasi", alisema Zitto.
Majimbo 6 yanamsubiri.
Akizungumzia
uchaguzi mkuu ujao, Zitto alisema atagombea nafasi ya ubunge kwa kuwa
umri wake hauruhusu kugombea nafasi ya rais, na kwamba jimbo
atakalogombea litawekwa wazi baada ya yeye kushauriana na washauri wake,
kwa kuwa majimbo zaidi ya sita nchini yanamtaka agombee.
"Nitasema
hapo baadaye ninagombea jimbo gani, kwa sababu majimbo mengi yananiita
nikagombee; Kawe wananitaka, Segerea, Kasulu, Kahama, hivyo nitazungumza
na wenzangu halafu nitasema nitagombea wapi"
alisema Zitto.
Alitetea
uamuzi wake wa kuhamia ACT, akisema ni uamuzi sahihi kwa kuwa chama
hicho kinaendana na kile alichokuwa anakipigania kwa miaka yote.
No comments:
Post a Comment