TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, March 31, 2015

Serikali yafafanua kuhusu bei za mafuta 

Naibu Waziri wa Fedha MWIGULU NCHEMBA
Serikali imetaja vigezo vinavyofuatwa katika kupanda na kushuka kwa bei za bidhaa kulingana na bei za Mafuta zinazopangwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji nchini - EWURA.
Naibu Waziri wa Fedha MWIGULU NCHEMBA ametaja vigezo hivyo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum CESILIA PARESSO na kuongeza kuwa Mchakato wa kushuka kwa Bei za Bidhaa hufanyika taratibu kulingana na hali halisi ya Soko.
Katika hatua nyingine naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi- PEREIRA AME SILIMA amesema kuwa Serikali inasikitishwa na vitendo vya Mauaji ya watu wenye UALBINO na kuwataka wananchi kuwafichua wale wote wanaohisia kufanya vitendo vya kinyama vya kuwauwa au kuwataka viungo.(TBC1

No comments:

Post a Comment