TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, March 31, 2015

Magari kumi ya bei ghali zaidi duniani

01. Lamborghini Veneno Roadster - $4.5 million
Name:  2015-lamborghini-veneno-r-2_600x0w.jpg
Views: 0
Size:  46.6 KB
02. Bugatti Veyron 16.4 Grand Sport Vitesse - $2.5 million
Name:  Vitesse_LoRes.jpg
Views: 0
Size:  681.2 KB
03. Koenigsegg Agera S - $1.5 million
Name:  koenigsegg-agera-s-hundra-front-right.jpg
Views: 0
Size:  1.29 MB
04. Hennessey Venom GT - $1.2 million

Name:  01-hennessey-venom-gt-spyder-cc.jpg
Views: 0
Size:  402.2 KB
05. Porsche 918 Spyder - $845,000
Name:  Porsche-918-2-672x372.jpg
Views: 0
Size:  184.1 KB
06. Rolls-Royce Phantom Extended Wheelbase - $298,900
Name:  2009-rolls-royce-phantom-extended-wheelbase-sedan-photo-261202-s-1280x782.jpg
Views: 0
Size:  102.1 KB

07. Ferrari F12berlinetta - $315,888
Name:  2013-ferrari-f12-berlinetta-front-three-quarters.jpg
Views: 0
Size:  1.02 MB
08. Bentley Mulsanne - $298,900
Name:  bentley-mulsanne-2.jpg
Views: 0
Size:  37.8 KB

09. Aston Martin Vanquish - $279,995
Name:  Aston-Martin-Vanquish-60.png.jpeg
Views: 0
Size:  449.1 KB


10. Mercedes-Benz CL65 AMG Coupe - $215,500
Name:  mercedes-benz-cl-65-amg-04.jpg
Views: 0
Size:  386.7 KB

MKUTANO WA MAWAZIRI WA FEDHA, WAENDELEA LEO JJIINI ADDIS ABABA


Mh.Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Harrison Mwakyembe akihutubia wajumbe wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango unaofanyika Mjini Addis Ababa –Ethiopia.

Naibu Katibu Mkuu –Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Nd. Armantius C.Msole (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr.Hamisi Mwinyimvua wakifuatilia hotuba ya Mh.Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr.Harrison Mwakyembe (Hayupo pichani) katika Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango wa Afrika unaofanyika Mjini Addis ababa – Ethiopia.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr.Hamisi Mwinyimvua akipata maelezo kuhusu utaratibu wa Mkutano kutoka kwa kamishina msaidizi wa Fedha za nje Bi.Judica Omari baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango unaoendelea Mjini Addis Ababa – Ethiopia. Katikati ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr.Albina Chuwa.(Muro)

Shanga za kale zagundulika nchini MISRI 

Wataalamu wa mambo ya kale mjini TEL AVIV, nchini ISRAEL, wamefukua na kubaini shanga za kale kutoka nchini MISRI, zilizofukuliwa katika mji huo.
Kwa mujibu wa wataalamu hao, shanga hizo ambazo ni za vito vya rangi ya bluu, zinaashiria kuwa wamisri, waliishi maeneo ya kaskazini zaidi mwa mashariki ya kati kuliko inayoonekana hivi sasa.
Shanga hizo zinaonekana kuwa na umri wa miaka elfu tano iliyopita.

SUMAYE: vijana jitokezeni kujiandikisha BVR 

Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu FREDERICK SUMAYE
Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu FREDERICK SUMAYE ametoa wito kwa wanawake na vijana nchini kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi Mkuu ujao.
Waziri Mkuu Mstaafu SUMAYE ametoa wito huo mjini KATESH wilayani HANANG mkoani MANYARA wakati akihutubia wananchi kutoka sehemu mbalimbali za wilaya hiyo ambapo pia amekemea vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.(TBC1)

Serikali yafafanua kuhusu bei za mafuta 

Naibu Waziri wa Fedha MWIGULU NCHEMBA
Serikali imetaja vigezo vinavyofuatwa katika kupanda na kushuka kwa bei za bidhaa kulingana na bei za Mafuta zinazopangwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji nchini - EWURA.
Naibu Waziri wa Fedha MWIGULU NCHEMBA ametaja vigezo hivyo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalum CESILIA PARESSO na kuongeza kuwa Mchakato wa kushuka kwa Bei za Bidhaa hufanyika taratibu kulingana na hali halisi ya Soko.
Katika hatua nyingine naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi- PEREIRA AME SILIMA amesema kuwa Serikali inasikitishwa na vitendo vya Mauaji ya watu wenye UALBINO na kuwataka wananchi kuwafichua wale wote wanaohisia kufanya vitendo vya kinyama vya kuwauwa au kuwataka viungo.(TBC1

Mwendesha mashitaka auawa Uganda 

Askari akikagua gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na Joan Kagezi
Watu wenye silaha wamemuua mwendesha mashitaka mkuu katika kesi ya watuhumiwa wa Kiislam wanaotuhumiwa kuua watu kadha katika mashambulio ya bomu mwaka 2010.
Mwendesha mashitaka huyo Joan Kagezi ambaye alikuwa kaimu mkurugenzi mwendesha mashitaka msaidizi nchini Uganda ameuawa kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa katika pikipiki wakati akiendesha gari kurudi nyumbani mjini Kampala.
Kesi inayoendelea inawahusu watu kumi na watatu wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji wa kikundi cha al-Shabaab.
Wanatuhumiwa kuua watu zaidi ya sabini wakati wakiangalia Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2010 katika mgahawa mmoja na katika uwanja wa klabu ya rugby.
Wiki iliyopita Marekani ilisema ilipata "habari za kuwepo uwezekano wa shambulio" katika maeneo ya mji ambayo raia wa mataifa ya magharibi wanakutana.
Serikali ya Uganda imesema Marekani ilionya juu ya uwezekano wa kuwepo kwa mtu anayejitoa mhanga akijaribu kuingia nchini humo.
Msemaji wa serikali amesema Uganda ilikuwa katika kitisho kwa sababu imechangia askari wengi katika jeshi la Umoja wa Afrika linalolinda amani nchini Somalia wakipambana na kundi la al-Shabab ndani ya Somalia.(BBC)

Ugomvi wa watoto ulianzia kwenye chakula.. mmoja wao akachukua bastola

Bastola 
Uliwahi kuipata story ya mtoto kwenye AMPLIFAYA na hapa kwenye millardayo.com ambapo mtoto huyo alimshoot mama yake ambaye alikuwa mjamzito, ukiangalia movie huwa wanaweka parental guide ambayo inaelekeza kwamba mtu mwenye umri wa kuanzia miaka mingapi anaruhusiwa kuiangalia.. haya matukio ni moja ya vitu ambavyo vinazuiwa mtoto asijifunze kutoka kwenye movies hizo.
Hii ya leo inahusu tukio lililotokea huko Florida Marekani, ambapo mtoto mwenye umri wa miaka 13, amemshambulia kaka yake mwenye umri wa miaka 16 pamoja na mdogo wake mwenye umri wa miaka 6, kwa kuwapiga na risasi halafu akajipiga mwenyewe.
Polisi wamesema watoto hao walikuwa peke yao nyumbani kwao wakati mama yao akiwa kazini wakaanza kugombania chakula, mtoto huyo akachukua bastola na kuanza kuwashambulia wenzake, kaka yake alipiga simu Polisi  ambao walifika eneo la tukio na kumkimbiza Hospitali lakini mtoto aliyewapiga risasi pamoja na mdogo wake walikutwa wameshafariki.
29906170001_4135510305001_video-still-for-video-4135458285001
Polisi wakiwa eneo la tukio

Maamuzi mapya ya Australia baada ya kujulikana Rubani aliiangusha ndege ya Ujerumani kwa makusudi

AIR AUSTRALIA LAUNCH BRISBANE 
Waziri mkuu msaidizi wa Australia Warren Truss ndio kaitangaza hii, na ni baada ya ajali ya ndege ya Ujerumani kuangushwa kwa makusudi na Rubani msaidizi huko Ufaransa na kuua watu wote ndani yake ambao walikua wanazidi 150.
Truss amesema mashirika ya ndege ya Australia ikiwemo Qantas na Virgin Australia wameanza kuyafanyia kazi mabadiliko ya usalama ambapo kuanzia sasa hakuna cha Rubani kubaki mwenyewe kwenye chumba cha Marubani, kama wako wawili na mmoja akawa anataka kutoka labda kwenda Toilet, inabidi muhudumu mmoja wa ndege aingie kwenye chumba hicho ndio rubani mmoja atoke.
Andreas Lubitz (27) rubani msaidizi aliyeiangusha ndege kwa makusudi.
Andreas Lubitz (27) rubani msaidizi aliyeiangusha ndege kwa makusudi.
Mabadiliko haya yameanza kufanyiwa kazi toka Jumatatu mchana March 30 2015 ambapo mwanzoni ilikua inaruhusiwa kwa Rubani mmoja kupaki kwenye chumba cha kurushia ndege.
Hii yote imekuja baada ya Rubani msaidizi kwenye ndege ya Ujerumani iliyoanguka Ufaransa kugundulika kwamba aliiangusha ndege kwa makusudi na ni baada ya Rubani mkuu kutoka nje ya chumba cha Marubani, alipotaka kurudi akakuta mlango umefungwa, yaani rubani msaidizi ndio kajifungia na akaiangusha ndege kwa makusudi.
Flight desk

Ubunifu mwingine kwenye mijengo mtu wangu.. Nimevutiwa sana na hizi PICHAZ

. 
Maajabu ya kuvutia.. yani zimetengenezwa nyumba na Hotel kwa ubunifu wa nguvu mtu wangu.
Nyumba za vioo, nyumba za miti.. Ziko nyingi hapa mtu wangu, unaweza kuzicheki zote.
.
Free Spirit Spheres, Canada. Utalii mwingine mzuri ndani ya nchi hiyo.
.
Boat Hotel. Hii Hotel vyumba vyake viko kama boti hivi, iko Visiwa vya Maldives, Asia.
La-Balade-Des-Gnomes-669x445
Trojan Horse Hotel. Kwa haraka haraka unaweza usijue hiki ni nini, lakini unaambiwa hii ni Hotel, hapo ndani kuna vyumba vya kulala na kila kitu kinaenda poa kabisa.
.
Ark Hotel, China. Wachina na teknolojia zao mtu wangu, hii Hotel imetengenezwa kwenye maji inaelea yani. Hapo unaweza kuona kwa juu inavyoonekana na kwa ndani ya maji pia.
.
Mirror Tree House, Sweden. Hapo panapoonekana kama mwanga mwekundu ni chumba cha Hotel yani, kimejengwa kwa vioo vitupu. Utakuwa na amani kweli kulala hapo?
.
Castle Hotel, Austria. Yani ni kama unauangalia Mlima hivi, karibu sana Austria mtu wangu.
.
Unadhani hii ni karavati ya barabarani? Hapana.. Ni vyumba vya Das Park Hotel, iko Austria. Vyumba nd’o viko hivyo yani. Mambo ya Ulaya Ulaya.
.
Umeielewa hii? Ni Hotel inayoitwa Airplane, iko Costa Rica. Hapo vipi mtu wangu, umevutiwa na hii?
attrap_reves_bubble_hotel
Bubble Hotel, unaweza kujionea hiii mtu wangu ukitembelea Ufaransa. Moja ya story zilizosikika March 2015 ni malalamiko ya baadhi ya watu kwamba hakuna usiri wowote ukiwa ndani ya chumba hicho cha Hotel.
.
Utajisikiaje kuwa kwenye hiki chumba cha kioo? Aina hii ya kioo ni kama kile kioo cha kujiangalizia.. mtu aliye nje haoni ndani. Hiki ni chumba cha Mirror Hotel, Berlin Ujerumani.
.
Hotel hii iko chini ya maji visiwa vya Fiji mtu wangu.
montana-magica-lodge_13
Magic Mountain Hotel, hii iko Panguipulli, Chile. Ukiiangalia kwa haraka ni kama Mlima uliozunguka na vichaka, hiyo ni Hotel mtu wangu.

Monday, March 30, 2015


BATIKI ZIPO SOKONI KARIBU KWA MAWASILIANO UKITAKA PIGA NAMBA 0656 507130
Kila aina unayoitaka unaweza kuipata cha kujifunga na cha kuchona

Si tu kwetu hata kwa wanaume wanaweza kupata za kwao za kushona







Wakazi wa kata ya kidete wilayani kilosa,Morogoro wako hatarini kukubwa na mafuriko na njaa

Wakazi wa kata ya kidete wilayani kilosa, Morogoro wako hatarini kukumbwa na mafuriko na baa la njaa kufuatia kingo za bwawa kidete lililojengwa ili kuzuia maji yanayotiririka kutoka milimani na kuzua maafa ya mara kwa mara kwenye wilaya hiyo kupasuka na kuharibu maelfu ya hekari za mashamba huku pia hali hiyo ikitishia usalama wa reli ya kati ambayo ni kiungo kikubwa cha usafiri wa abiria na mizigo ndani na nje ya nchi.
Hofu ya kuzuka kwa mafuriko hasa kipindi hiki cha masika inaibuka kwa wakazi wa kata hiyo baada ya kingo za bwawa la kidete linalodaiwa kutafuna zaidi ya shilingi bilioni 3.5 kubomoka wakati ujenzi wake ukiendelea hali inayosababisha maji kutiririka kwa wingi na kuingia katika maeneo ua makazi na tayari yameshakwisha haribu maelfu ya hekari za mashamba na endapo mvua zitaendelea kunyesha kwa wingi maji hayo huenda yakaleta madhara kwenye reli ya kati amabayo inapita wilayani humo.
Mbali na kuzua hofu ya janga la mafuriko na baa la njaa kutokana na kuvunjika kwa bwawa hilo ambalo asili yake lilijengwa na wajerumani ili kuzuia maji yasiharibu miundombinu ya reli lakini pia lilikuwa likitoa ajira ya uvuvi kwa vijana ambao hapa wanaonyesha masikitiko yao ya kukosa kipato.
ITV inazungumza na mwenyekiti wa kijiji cha kidete stesheni yusuph bakari ambaye mradi wa bwawa hilo unatekelezwa katika eneo lake analalamikia siasa kuingizwa kwenye ujenzi wake ambao tayari umetafuna mabilioni ya fedha za walipakodi huku kukiwa hakuna dalili zozote za kukamilika kwa wakati. (CHANZO:ITV

Vurugu Lugha za Matusi zatawala kwenye semina ya wabunge Mkoani Dodoma


Vurugu ,matusi na lugha za kejeli ni miongoni kati ya mambo yaliyotawala semina ya wabunge kuhusiana muswada wa sheria ya kutambulika hukumu zitakazokuwa zikitolewa na mahakama za kadhi hapa nchini wa mwaka 2014/2015.
Ni sehemu ya hali ilivyokuwa wakati wabunge waliposhindwa kuvumuliana na kuheshimiana walipokuwa wakichangia mara baada ya Jaji Robert Makaramba alipowasilisha mada kuhusiana na muswada huo hali iliyolazimu ulinzi kuimarishwa ndani ya ukumbi huo kwa hofu kwamba huenda waheshimiwa wabunge hao wakatwangana makonde na ndipo semina ilipoendelea.
Mbunge wa kuteuliwa, Kassim Issa mbunge baraza la wawakilishi,
Dakika chache baadaye ikafika kipindi cha kila mtu kumtafuta mbaya wake ama suluhu ya anachokiamini huku lugha za kutishana zikitawala.
Wakihitimisha semina hiyo muwasilisha mada Jaji Robert Makaramba pamoja na Waziri mkuu Mh.Mizengo Pinda wamesema ujumbe umefika na mapungufu yaliyoonekana yatafanyiwa kazi

MWAKIFWAMBA KITANZINI, ATAKIWA KUACHIA NGAZI

 KIBANO! Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (Taff), Simon Mwakifwamba amejikuta kwenye wakati mgumu kwenye mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika kwenye ofisi za shirikisho zilizopo Kinondoni, Dar akitakiwa kuachia ngazi.
Habari kutoka kwa sosi aliyekuwa ndani ya kikao hicho zilinyetisha kwamba, wanachama wa shirikisho hilo walisema wamechoshwa na rais huyo na kwa sababu muda wake umekwisha, alitakiwa kuachia ngazi.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (Taff), Simon Mwakifwamba
"Mwakifwamba amebanwa sana, ametakiwa kuachia ngazi na kueleza amefanya nini kwenye uongozi wake ikiwa ni pamoja na kueleza gari la shirikisho amelipeleka wapi kwani tangu apate nalo ajali hata katibu wake hajui limekwenda wapi," alisema sosi huyo.
Baada ya habari hizo kutua kwenye meza ya Ijumaa Wikienda, mwanahabari wetu alifika ofisini kwa Mwakifwamba na kukuta kikao kikiendelea.
Baada ya kikao hicho mwandishi wetu alipata fursa ya kuzungumza na Mwakifwamba ambaye alikiri kuulizwa kuhusiana na gari ambapo aliwaambia lipo gereji.