ZANZIBAR MIDIA CORPORATION LTD YAANDA TAMASHA LA WASANII WA ZANZIBAR
Mwenyekiti
wa Tamasha la tunzo za wasanii bora Zanzibar mwaka 2014/15 Seif Mohd
Seif akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya tamasha
hilo Ofisini kwake mtaa wa Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Picha
Na Makame Mshenga –Maelezo Zanzibar.
Mratibu
wa Tamasha hilo Ramadhani Senga akijibu masuala ya waandishi wa habari
kuhusu tunzo za mwaka huu katika mkutano uliofanyika Jengo la Zanzibar
Media Corporation Limited mtaa wa Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya
waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo katika jengo la Zanzibar
Media Corporation Limited wakifuatilia mazungumzo hayo.
Meneja
Masoko wa Zanzibar Media Corporation Limited Said Khamis akitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa habari katika Mkutano wa maandalizi ya
Tamasha la tunzo za wasanii bora Zanzibar mwaka huu uliofanyika jengo la
Zanzibar Media Cortporation Limited mtaa wa Mombasa. Picha Na Makame
Mshenga –Maelezo Zanzibar.
Taratibu
za Tamasha la kuwatafuta wasanii bora wa Zanzibar (Zanzibar Music
Awards) zinazosimamiwa na Kampuni ya Zanzibar Media Corporation
inayomiliki kituo cha Zenj Fm radio na kitengo cha Zenj Entertainment
kwa mwaka 2014/2015 zimeanza rasmi leo.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika jengo la Zanzibar Media Corporation, mtaa
wa Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Tamasha hilo
Seif Mohd Seif amesema maandali yamekamilika. Amesema tunzo hizo ambazo
zinalengo la kuwanyanyua wasanii wa Zanzibar kibiashara zitafikia kilele
chake siku ya Ijumaa tarehe 27.2.2015 katika ukumbi wa Salama Hoteli ya
Bwawani.
"Lengo la
tunzo hizi ni kuweza kuwatangaza wasanii wetu wa hapa Zanzibar
kibiashara, kuona thamani ya kazi zao na mchango wa sanaa zao
unavosaidia jamii kuipa taaluma kupitia sanaa hizi," alisisitiza Seif
Mohd Seif.
Ameongeza
kuwa tamasha la mwaka huu ambalo ni la nane, kama yalivyo matamasha
yaliyopita yanasaidia kuinua sekta ya utalii kutokana na wageni mbali
mbali kuhudhuria. Ametoa shukrani kwa wasanii wote wa Zanzibar kwa
kuonyesha moyo wa kuziimarisha kazi zao ambazo zinakuwa na mvuto kwa
jamii kwa kuendeleza sanaa nchini.
Pia
ameipongeza Kamati ya majaji kwa kazi kubwa waliyofanya ya kupitia kazi
za wasanii, na wadau mbali mbali kutoka vyombo vya habari vya Zanzibar
ikiwemo Baraza la sanaa kwa michango mikubwa waliyotoa kufanikisha
maandalizi ya Tamasha hilo.
Mwenyekiti
wa Zanzibar Music Award amesema katika Tamasha hilo jumla ya makundi 18
yatawania tunzo hizo kwa wasanii wa Zanzibar pekee.
Ameyataja
makundi hayo kukwa ni Video bora ya mwaka muziki wa kizazi kipya, video
bora ya mwaka taarab ya kisasa, Mwanamuziki bora wa mwaka wa hip hop,
Mwanamuziki wa mwaka wa R&B, Mwanamuziki bora wa Afro pop na
Mtaarishaji bora wa mwaka.
Wengine
ni Mwanamuziki bora wa kiume na wa kike taarab ya kisasa, Wimbo bora wa
taarab ya kisasa ya mwaka, Mwanamuziki bora wa kiume na wa kike taarab
asilia, Mwanamuziki bora wa kike na kiume muziki wa kizazi kipya na
wimbo bora wa mwaka wa kizazi kipya.
Katika
makundi hayo pia kutakuwa na tunzo ya Mwanamuziki bora chipukizi wa
mwaka, Mwanamuziki bora wa mwaka na Mshairi bora wa mwaka. Seif Mohd
Seif amewataka watu wote wanaopenda kushiriki tunzo za mwaka huu kuwa
upigaji wa kura umeanza rasmi leo Jumapili na utamalizika siku ya
Jumatano tarehe 25.2.2015 na matangazo ya kupiga kura yatarushwa na
vyombo mbali mbali na katika Gazeti la Nipe Habari na kupitia website
yaowww.zenjifmradio.com
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment