Burundi: mahakama yaamua Bob Rugurika kusalia jela
Mahakama
ya jiji la Bujumbura imechukua uamzi wa kumbakiza jela mwanahabari Bob
Rugurika, akiwa pia mkurugenzi wa redio RPA, inayosikilizwa na watu
wengi nchini Burundi na baadhi ya maeneo ya nchi jirani.
Uamzi huo
wa mahakama umekua unasubiriwa ndani ya masaa 48 tangu Jumatatu wiki
hii, baada ya mkurugenzi wa redio RPA, kufikishwa mbele ya majaji,
katika jela la mkoa wa Muramvya anakozuiliwa. Wanasheria wake wamebaini
kwamba watakata rufaa dhidi ya uamzi huo wa Mahakama. Umoja wa Ulaya,
Marekani, mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu wameitaka serikali
kumuachilia huru mwanahabari huyo, kwani hana hatia, huku wakiomba
uchunguzi uanzishwe kuhusu watawa 3 kutoka Italia waliouawa mwanzoni mwa
mwezi Septemba.
Bob
Rugurika alikamatwa na kupelekwa katika jela kuu la Mpimba Jumanne
Januari 20 jioni, baada ya kuitika hati iliyotolewa na afisa katika
ofisi ya mwendesha mashitaka katika manispaa ya jiji la Bujumbura,
Emmanuel Nkurikiye, ambaye alimtaka amfikishe mikononi mwa vyombo vya
sheria, mtu mmoja aliyekiri kuhusika na mauaji ya watawa watatu kutoka
Italia waliouwawa tarehe 7 na 8 Septemba mwaka 2014, katika wilaya ya
Kamenge, kaskazini mashariki mwa mji wa Bujumbura.
Redio RPA
iliendesha uchunguzi kuhusu mauaji hayo, na kwa muda wawiki kadhaa
redio hio ilikua ikiweka wazi matokeo ya uchunguzi wake, ambapo mtu huyo
aliyekiri kuhusika katika mauaji hayo, aliwanyooshea kidole baadhi ya
maafisa wakuu katika Idara ya Ujasusi ya Burundi pamoja na polisi,
akibaini kwamba wao ndio waliomuagiza akishirikiana na watu wengine
(ambao aliwataja majina) kutekeleza mauaji ya watawa hao.
Mtu huyo
aliyehojiwa na redio RPA, alimtaja mkurugenzi wa zamani wa Idara ya
Ujasusi ya Burundi, jenerali Adolphe Nshimirimana, akibaini kwamba ni
mmoja kati ya maafisa wa Idara ya Ujasusi na polisi walioandaa mpango
huo wa kuwamalizia maisha watawa hao kutoka Italia.
Hata
hivyo katika uchunguzi wake, RPA ilibaini kwamba ilijaribu kuwatafuta
watu wote waliotajwa katika kesi hiyo, baadhi walikanausha tuhuma dhidi
yao, na wengine walisema kwamba wanasubiri uchunguzi wa vyombo vya
sheria vya Burundi.
Akihojiwa
na afisa wa Ofisi ya mashitaka, Bob Rugurika alisema, kama chombo cha
habari, na kulingana na sheria za uandishi wa habari, RPA iliendesha
uchunguzi wake bila hata hivyo kuingilia vyombo vya sheria katika
uchunguzi wake, ili kujaribu kutoa mwanga kuhusu mauaji hayo.
Afisa wa
Ofisi ya mashitaka anamtuhumu Bob Rugurika kwamba hakutoa ushiriki wake
kwa vyombo vya sheria, kuingilia kazi za vyombo vya sheria wakati kesi
ikiwa katika hatua ya uchunguzi, na kushiriki katika mauaji ya watawa
hao watatu kutoka Italia.
Mkurugenzi
wa redio RPA anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela, iwapo
atapatikana na hatia. Baada ya mauaji ya watawa hao, polisi ya Burundi
ilimkamata mtu mwenye ugonjwa wa akili, ikimtuhumu kuhusika katika
mauaji ya watawa watatu waliouawa tarehe 7 na 8 septemba mwaka 2014
wilayani Kamenge mjini Bujumbura.
Redio RPA imekua ikiendelea kurusha matokeo ya uchunguzi wake, licha ya kuwa mkurugenzi wake anazuiliwa jela.
Kanisa kuu la mjini Bujumbura, Burundi.
flickr
Kanisa
Katoliki nchini Burundi inaendela kuomba mkurugenzi huyo wa redio RPA
aachiliwe huru, huku ikiomba vyombo vya sheria vya Burundi kuanzisha
uchunguzi wa kina ili waliohusika katika mauaji hayo wajulikane, na
waadhibiwe kwa mujinu wa sheria.CHANZO:R.F.I
No comments:
Post a Comment