Ajira 40,735 Zazalishwa Ndani ya Miezi Mitatu
Ajira 40,735 zimezalishwa ndani ya miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka jana na kufanya jumla ya ajira 173,787 kupatikana kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana.
Wizara
 ya Kazi na Ajira imesema ongezeko hilo la ajira limejitokeza katika 
maeneo makuu mawili ikiwemo ajira serikalini ambazo ni 2,652 sawa na 
asilimia 6.5 na ajira kupitia sekta rasmi binafsi ambazo ni 38,083 sawa 
na asilimia 93.5.
Akizungumza
 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Wizara hiyo, 
Ridhiwan Wema alisema takwimu hizo zinaonesha kwamba sekta binafsi 
imeendelea kuwa mhimili wa uzalishaji wa ajira nchini kutokana na 
serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya waajiri kuongeza fursa za
 ajira kwa Watanzania.
“Katika
 kipindi cha nusu mwaka  sekta binafsi rasmi ambayo ndiyo mwajiri mkuu 
ilizalisha ajira 173,787 kupitia uwekezaji binafsi ambapo uwekezaji 
kupitia ujenzi zilizalishwa ajira 107,527, uwekezaji kupitia  Kituo cha 
Uwekezaji (TIC) ajira 34,184 na Sekta ya Mawasiliano ajira 342” alisema.
Alisema
 hatua zinazochukuliwa kwa sasa ni pamoja na kufanya marekebisho ya Sera
 ya Ajira ya 2008, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Namba 6,2004, 
Sheria ya Taasisi za Kazi namba 7,2004 pamoja na kutunga sheria Mpya ya 
Ajira za Wageni ambayo imelenga kulinda ajira za Watanzania, kuboresha 
mazingira ya biashara na kuhamasisha uwekezaji.
Alishukuru
 wadau mbalimbali kwa ushirikiano wao kwa kutoa taarifa za ajira kwa 
wakati. Alitoa mwito kwa waajiri wote nchini kutoa ushirikiano katika 
ukusanyaji taarifa za soko la ajira.
“Taarifa
 hizi zimelenga kuiwezesha serikali kujua hali ya ajira nchini na 
kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuwezesha serikali kupanga 
matumizi sahihi ya nguvu kazi nchini,” alisema.

No comments:
Post a Comment