TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, February 17, 2015

Watu 50 Waliohusika na Vurugu za Geita Wakamatwa.....Mkuu wa Wilaya Aagiza Walimu wakuu Walioruhusu Wanafunzi Kufanya Fujo Washushwe Vyeo 


Zaidi ya watu 50 wamekamatwa na jeshi la polisi kufuatia vurugu kubwa iliyotokea katika mji wa katoro mkoani Geita.

Chanzo cha vurugu hizo ni mgomo wa wanafunzi wa shule za msingi kilimani, Mkapa na Ludete ambapo walilala katikati ya barabara, kushinikiza kuwekewa matuta kutokana na matukio ya ajali ya mara kwa mara hivyo kutishia usalama wao.
 
Hata baada ya kuwekewa matuta kuzuia ajali vurugu hizo zilipamba moto kutoka kwa wanafunzi na kuingia watu wazima na kuanza kupiga mawe magari yote yaliyokuwa yakipita barabarani ambapo zaidi ya magari 7 yameharibiwa vibaya na watu kujeruhiwa.
 
Baada ya muda kuonekana hali imetulia,magari yaliruhusiwa kuondoka hata hivyo hali haikuwa shwari ambapo magari yote yalirudi katika kituo cha polisi katoro kwa usalama zaidi.
 
Mkuu wa Wilaya ya Geita ameagiza walimu wakuu wote wa shule za msingi zilizohusika na uanzishwaji wa vurugu hizo kushushwa vyeo vyao na hatua mbalimbali za kisheria zizingatiwe.

No comments:

Post a Comment