Watanzania sasa Kupatiwa Viza Huko Huko India
Wasafiri kutoka Tanzania kwenda India kwa shughuli za matibabu na biashara wataruhusiwa kupata visa wafikapo nchini humo.
Hayo
yalisemwa na Balozi wa India nchini, Debnath Shaw wakati akijibu
maswali ya wafanyabiashara wa kitanzania wakati wa mkutano baina ya
wafanyabiashara wa ndani na wenzao kutoka jimbo la Gujarat India.
Alisema: “Tutahakikisha tunafanya utaratibu huo na utaanza siku za usoni ili kupunguza usumbufu wanaoupata Watanzania waendao India”.
Kwa
upande wake, Ofisa Mkuu Mtendaji wa Global Investors Consultstion
Center (GICC), Shainul Bhanji alisema kutokana na ripoti ya Benki ya
Dunia Tanzania imeonekana kuwa ni nchi yenye mazingira mazuri ya
biashara kwani ripoti inaonesha Tanzania inaendelea kushika nafasi nzuri
ukilinganishwa na nchi jirani za Kenya na Uganda.
“Tanzania
ilikuwa nafasi ya 142 kati ya 180 kwa mwaka 2011 lakini sasa imepanda
hadi nafasi ya 131 huku Kenya ikiwa katika nafasi ya 136 na Uganda
nafasi ya 132,” alisema Bhanji.
Naye
Rais wa Taasisi ya Wenye Viwanda toka Jimbo la Gujarat India Amit Patel
alisema kwa sasa India ni nchi ya nne kwa ukubwa kwa nchi
zinazofanyabiashara kwa Afrika na wana uhakika kuwa watafanyabiashara
kuzidi China, Marekani na Ulaya.
Alisema
Serikali ya India imeahidi kutoa mikopo ya masharti nafuu ya bilioni 6
mwaka huu kwa nchi za Afrika ili kuboresha miundombinu na mazingira ya
kufanyabiashara.
Naye
Mwenyekiti wa wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda nchini Francis
Lukwaro alisema mkutano utasaidia wafanyabiashara wa Tanzania kujifunza
mambo mapya ya kibiashara kutoka India.
Alisema
kwa upande wa Tanzania kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa
wafanyabiashara hawa kwani wengi wao ni wafanyabiashara wakubwa na
wameendelea.
No comments:
Post a Comment