Fedha Zakwamisha kukamilika Mradi wa DART
Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) unakabiliwa na changamoto ya kifedha katika ujenzi wa miundombinu, kutokana na ongezeko la mahitaji ya fedha za kuukamilisha.
Bunge
lilielezwa kwamba ongezeko la mahitaji ya fedha za kukamilisha mradi
huo ni Sh bilioni 64.7, ambazo kati yake Sh bilioni 20.6 ni ongezeko la
mishahara na Sh bilioni 44.1 ni ongezeko la kazi na madai mengine.
Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dk Athuman
Mfutakamba alisema hayo jana wakati akiwasilisha taarifa ya mwaka ya
kamati kuanzia Januari 2014 hadi 2015.
Kamati
hiyo imeishauri serikali kufanya jitihada za makusudi, kuhakikisha
mradi unaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa na fedha yote
inayohitajika kukamilisha hatua mbalimbali za mradi, zinatengwa na
kupelekwa hatua zikamilike kwa wakati.
Kwa
mujibu wa Mfutakamba, inadaiwa ongezeko hilo limefanya mkandarasi
kutoonesha utayari wa kuanza kazi katika barabara ya Msimbazi kwa hofu
ya kutokuwepo kwa fedha za kumlipa.
Changamoto
nyingine ambayo wabunge walielezwa kwamba inakabili mradi, ni uharibifu
wa miundombinu ambao baadhi ya wananchi na wafanyabiashara ndogo
huvamia maeneo ya ujenzi yanayoendelea.
Vile vile kumekuwapo tabia ya wizi wa samani za barabara, mifuniko ya maji ya mvua, maji taka na huduma nyingine.
No comments:
Post a Comment