NSSF YAANZA MCHAKATO WA KUWASAKA WENYE VIPAJI VYA MPIRA WA MIGUU
Itakumbukwa
kuwa mnamo tarehe 26/01/2015 Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF) lilisaini mkataba maalum na timu ya Real Madrid ya Nchini
Hispania ya kuanzisha na kuendesha kituo cha michezo (NSSF- REAL MADRID
Sports Academy) kwa lengo la kuibua, kuendeleza na kukuza vipaji kwa
mpira wa miguu.
Shirika
la NSSF litajenga kituo hicho katika eneo la Mwasonga Kigamboni nje
kidogo ya mji wa Dar es Salaam na wataalamu kutoka timu ya Real Madrid
watatoa mafunzo kwa vijana wa umri wa miaka13 hadi 19 kwa madhumuni ya
kukuza mpira wa miguu nchini, kupata wachezaji bora wanaouzika nje na
ndani ya nchi pamoja na kulipatia mapato shirika na nchi kwa ujumla .
Akizungumza
na Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya Habari Nchini, Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika hilo Dr. Ramadhani K. Dau alisema mradi huo ukiwa kama
sehemu ya uwekezaji wa NSSF ulianza maramoja baada ya kusaini mkataba.
NSSF
imeanza utaratibu wa kuwabaini vijana walengwa ambapo kwa kuanzia
utafutaji wa vipaji vya mpira wa miguu utaanzia mkoa wa Dar es Salaam
kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 14. Utafutaji wa vipaji
utafanyika kiwilaya kwa Wilaya za mkoa wa dar es salaam na utakuwa
unafanyika katika viwanja vya Karume. Zoezi hilo litakuwa linafanyika
kati ya saa 1 asubuhi hadi saa 9 alasiri kwa tarehe zilizoainishwa.
Uandikishaji
wa washiriki utakuwa unafanyika siku za mwisho wa wiki ili kutoathiri
wanafunzi watakaopenda kushiriki na utaanza rasmi tarehe 14 na 15,na
tarehe 22 na 23 Februari 2015, na kufuatiwa na michezo ya majaribio
tarehe 28 Februari,na Tarehe 1 Machi 2015 kwa wilaya zote za mkoa wa Dar
es salaam ambapo kituo kitakuwa viwanja vya Karume kuanzia saa moja
asubuhi hadi saa 9 alasiri.
Zoezi la
Uandikishaji halitahusisha gharama zozote kwa washiriki, na uandikishaji
wa washiriki utafanyika kwa kujaza fomu maalum na kupewa namba ya
ushiriki na kila mshiriki atapata fursa ya kucheza katika awamu mbili za
dakika 30. Kwa kuanzia washiriki watatakiwa kuja na vifaa vyao vya
michezo.
Zoezi la
awali litafanywa na wataalam wa ndani ya nchi ambapo Vijana 500 kati ya
wote watakaofanyiwa majaribio wataingia katika awamu ya pili ya
majaribio na watadahiliwa na wataalamu kutoka Klabu ya Real Madrid na
hatimaye kupatikana vijana 30 amabo ndio wataingia katika shule maalum
ya mafunzo kwa awamu ya kwanza.
Wakati wa
uandikishwaji washiriki watatakiwa kuja na wazazi/walezi wao wakiwa na
vitambulisho vyao,na kijana husika awe na Cheti halisi cha kuzaliwa na
kopi yake pamoja na picha mbili za pasport rangi ya blue.Muda wa
uandikishaji na majaribio unaweza kuongezwa kulinagana na mahitaji.
Shirika
la NSSF linatoa wito kwa vijana kujitokeza kwani ni fursa kwao ya kuweza
kujiendeleza kimichezo na kujiajiri katika tasnia hiyo
No comments:
Post a Comment