Mtoto wa wazazi watatu kuzaliwa Uingereza
Wabunge
wa bunge la Uingereza wameunga mkono sheria inayoruhusu uzaaji wa wa
watoto wenye vinasaba, DNA kutoka kwa wanawake wawili na mwaume mmoja,
katika tukio la kihistoria.
Uingereza kwa sasa itakuwa nchi ya kwanza kuweka sheria zinazoruhusu watoto wenye vinasaba vya watu watatu tofauti.
Katika
kura iliyopigwa katika bunge la Commons, wabunge 382 waliunga mkono
muswada huo wa sheria na wabunge 128 walipinga mbinu inayozuia magonjwa
ya kijenetiki kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Wakati wa mjadala huo, mawaziri wamesema mbinu hii ni "mwanga kwa safari ndefu ya giza" kwa familia kupata watoto.
Upigaji
kura zaidi unahitajika katika baraza la bunge la juu, maarufu kama House
of Lords. Iwapo kila kitu kitakwenda sawa, basi mtoto wa kwanza wa
teknolojia hii atazaliwa mwaka ujao.
Watetezi
wa mpango huu wanasema uungwaji mkono wa sheria hii "ni habari njema kwa
maendeleo ya tiba" lakini wakosoaji wanasema wataendelea kupinga mpango
huu ambao una mashaka mengi kuhusu maadili na usalama katika uzazi huu.
Makisio yanasema watoto 150 wanaopatikana kutokana na vinasaba vya watu watatu watazaliwa kila mwaka.
Waziri
Mkuu wa Uingereza David Cameron anasema: "Hatuzungumzii Mungu hapa,
tunahakikika kuwa wazazi wawili ambao wanataka mtoto mwenye afya
wanaweza kumpata."
Mpango
huu ambao umebuniwa Newcastle, utasaidia wanawake kama Sharon Bernardi,
kutoka Sunderland, ambaye alipoteza watoto wote saba kutokana na ugonjwa
wa mitochondrial.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment