TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, February 3, 2015

Rais wa Ujeruman atua nchini, aja na wafanyabiashara 14 

Rais Joachim Gauck wa Ujerumani ameambatana na ujumbe mzito wa wafanyabiasha 14 katika ziara yake ya siku tano nchini.
Rais huyo aliyewasili jana usiku nchini atazungumzia fursa za uwekezaji katika kilimo, biashara na usarifishaji. Pia kuhusiana na mradi wa uzalishaji wa mbolea unatakaofanywa baina ya Kampuni ya Ferrostaal GmbH pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), yenye uwezo wakuzalisha mbolea tani 1.3 milioni kwa mwaka.
Akitoa taarifa ya ujio wa rais huyo jana, jijini Dar es Salaam, balozi mdogo wa Ujerumani nchini, John Reyels alisema baada ya kuwasili, kiongozi huyo atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Kikwete ambayo yatalenga mambo mbalimbali ikiwamo suala la uwekezaji.
Licha ya kuwa, Balozi Reyels hakufafanua zaidi kuhusiana na kile atakachozungumza Rais Gauck, lakini alisema kuwa kupitia wajumbe 14 ambayo ni wafanyabiashara wakubwa wa nchini humo wataangazia fursa za uwekezaji nchini na mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa kati ya 2019/2020.
Wajumbe hao ni kati ya wajumbe 90 waliyoongozana na Rais Gauck katika ziara yake nchini ambayo ataifanya kwa siku tano na kurejea Ujerumani.
Rais huyo, ambaye anatembela Tanzania kwa mara ya kwanza kutokana na mwaliko wa Rais Kikwete, pia atatembelea Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front.
"Wakati ziara yake kanisani hapo Rais Gauck atakuwa na mazungumzo na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Alex Malasusa,"alisema Balozi Reyels.
Balozi Reyels, alieleza sababu ya Rais huyo kutembelea kanisa hilo na kusema kuwa, "Kanisa hilo linahistoria kubwa na Ujerumani kwani lilijengwa na Wajerumani takriban miaka 100 iliyopita...hata hivyo Rais mwenyewe aliwahi kuwa mchungaji kabla ya kuwa na wadhfa alionao sasa

No comments:

Post a Comment