TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, February 8, 2015

UBUNIFU WA KUVUTIA WATEJA KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA MASCUT OMAN 

Bunduki ni miongoni mwa zana zinazotumika katika ngoma ya Asili kutoka nchini Moroko. Pichani Wasanii hao wakitumbuiza nje ya banda lao kuvutia wateja kujionea bidhaa mbalimbali za nchi yao katika maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,ubunifu na utamaduni.
Wasanii wa Ngoma za Asili kutoka Tanzania wakitumbuiza nje ya Mlangoni wa Banda lao la Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni Mascut nchini Oman. Utumbuizaji wa ngoma ni mfumo wanaoutumia katika kuwavutia na kuwafurahisha Wateja kuingia katika Banda la Tanzania kwenye Maonesho hayo. Pichani ni Ngoma ya Msewe yenye asili ya Zanzibar.
Warembo kutoka Thailand wakiwa Wametulia nje ya Mlango wa Banda lao ikiwa ni ubunifu wa kuwavutia na kuwafurahisha Wateja wanaoingia katika Banda lao kujionea bidhaa mbalimnali za nchi yao katika Maonesho ya Kimatifa ya Sanaa,ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Mascut-Oman.Picha na Faki Mjaka

No comments:

Post a Comment