Taiwan: ndege yaanguka mtoni ikiwa na abiria 58
Baada ya
ajali ya ndege iliyogharimu maisha ya abiria 54 mwezi Julai mwaka
uliyopita nchini Taiwan, ndege nyingine ya shirika la ndege la TransAsia
imeanguka asubuhi mapema Jumatano wiki hii katika mji mkuu wa nchi
hiyo, Taipei.
Kwa jumla
ya abiria 58 waliokua ndani ya ndege hio, 11 wanashukiwa kufariki,
takribani 18 wameokolewa, huku 30 wakiwa bado wamenasa katika ndege
hiyo.
Ngede
hiyo ilikua ikitokea katika uwanja ndege wa Songshan mjini Taipei,
ikielekea katika kisiwa cha Kinmen kwenye mwambao wa China. Muda mchache
baada ya kuruka, kwenye saa tano asubuhi (saa za Taiwan), ndege hiyo
ilijigonga kwenye daraja kabla ya kuanguka katika mto Keelung, kwa
sababu ambazo bado hazojajulikana.
Kwa
mujibu wa Mamlaka ya usafiri wa anga, ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 58
ikiwa ni pamoja na wafanyakazi watano. Wakati huu, abiria 18
waliokolewa na kusafirishwa hospitalini, amesema afisa wa shughuli za
uokozi kwenye mtandao.
Kwa
mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP, watu kumi na moja
wamefariki na thelathini wengine zaidi ya thelathini bado wamenasa
katika ndege, wakati ambao shughuli za uokozi zikiendelea ili kuwaondoa
abaria ambao bado wamenasa katika ndege hiyo ambayo inaendelea kuzama.
Hii ni
ajali ya pili katika kipindi cha miezi saba kwa shirika la ndege la
Taiwan. Julai 23, ndege ya shirika la la ndege la Taiwan TransAsia
ilianguka katika kisiwa cha Penghu, magharibi mwa Taiwan, wakati dhoruba
Matmo ilikua ikipiga katika ukanda huo. Kwa jumla ya abiria 58, 48
walifariki, ikiwa ni pamoja na raia wawili wa Ufaransa.CHANZO:R.F.I
No comments:
Post a Comment