HUAWEI NA UMOJA WA AFRIKA ZASAINI MAKUBALIANO
Makamu wa
Rais wa kampuni ya Huawei katika idara inayohusika na mahusiano ya
serikali Ulimwenguni, Bw. David Harmon (wapili kushoto) akipeana mkono
na Makamu Mweyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Bw. Erastus Mwencha
(wapili kulia), mara baada ya kusaini makubaliano yatakayosaidia
kuongeza ushirikiano baina yao katika kuimarisha maendeleo katika
miundombinu ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano (teknohama).
Hafla ya kusaini makubaliano hayo ilifanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande zote mbili.(V.S)
Kampuni
ya Huawei Technologies inayoongoza katika sekta ya habari na mawasiliano
duniani, imesaini makubaliano (MoU) na Umoja wa Afrika (AU),
makubaliano yatakayosaidia kuongeza ushirikiano baina yao katika
kuimarisha maendeleo katika miundombinu ya teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (teknohama).
Makubaliano
hayo yalisainiwa hivi karibuni mjini Addis Ababa, Ethiopia kwenye
Mkutano wa AU wa mwaka 2015 ambao pamoja na mambo mengine ulijadili pia
namna ya kuimarisha uelewa wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(teknohama) kwa nchi wanachama sambamba na kujenga uwezo wa juu katika
maendeleo ya miundombinu ya teknolijia hiyo.
Akizungumza
kwenye mkutano huo, Makamu mweyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika
Bw. Erastus Mwencha alisema maendeleo ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (teknohama) yana msaada mkubwa kwa ukuaji wa uchumi
ulimwenguni na pia ni nguzo muhimu katika kuleta madadiliko chanya
kwenye setka mbalimbali.
"Maendeleo
ya teknolojia hii yataleta mabadiliko makubwa sana katika sekta
mbalimbali na ndio maana tunatafuta washirika wanaoweza kufanya kazi na
sisi ili kufanikisha hilo. Huawei kama kampuni imara kwenye teknolojia
hiyo tunaamini pia itakuwa ni msaada mkubwa itakapo shirikiana na
sisi...tunafurahi kuwa nao kwenye huu mradi,'' alisema Mwencha.
Kwa
upande wake, Makamu wa Rais wa kampuni ya Huawei katika idara
inayohusika na mahusiano ya serikali Ulimwenguni, Bw. David Harmon
alisema kampuni yake ina nia yakukuza kimataifa maendeleo sekta ya
teknohama na ndiyo maana kwa muda mrefu imekuwa ikisaidiana na serikali
mbalimbali katika kuimarisha miundombinu inayohusiana na sekta hiyo.
"Huawei
ina jukumu la kuhakikisha tunashikirikaina na washirika wetu kwenye
nyanja zote za teknohama ili kujenga Afrika bora yenye kushikamana, kwa
sababu tunaamini kwamba teknolojia ICT, hasa mawasiliano ya simu ni
nguzo muhimu si tu kwa Afrika bali ulimwenguni wote.
"Kwa
miaka yetu 17 ya uzoefu katika sekta ya teknohama sambamba na mtandao wa
kimataifa ulimwenguni kote ina maana kwamba Huawei ipo katika nafasi
nzuri ya kushiriki kwenye namna bora ya kutafuta ufumbuzi kwa masuala ya
teknohama. Tupo tayari kubadilishana uzoefu wetu na Umoja wa Afrika, "
Harmon aliongeza.
No comments:
Post a Comment