TIC YAKUTANA NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA KUTOKA NCHINI UJERUMANI
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (wa pili
kushoto) akizungumza katika mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na
ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la
kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na
Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo
hicho,jijini Dar es salaam.Ujumbe huo unaongozwa na Waziri wa Masuala ya
Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig (wa pili
kulia)
Mratibu
wa Uwekezaji wa Kimataifa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Zacharia
Kingu akifafanua jambo wakati akiwasilisha taarifa ya uwekezaji katika
maeneo mbali mbali nchini wakati wa mkutano maalum kati ya Uongozi wa
TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la
kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na
Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo
hicho,jijini Dar es salaam.
Ujumbe wa
wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani pamoja uongozi wa TIC
ukifatikia kwa makini taarifa ya uwekezaji iliyokuwa ikitolewa na
Mratibu wa Uwekezaji wa Kimataifa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC),Zacharia Kingu (kushoto).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki
(katikati) akitoa ufafanuzi wa maswala mbali mbali ya uwekezaji kwa
ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani waliotembelea kituo
hicho jana jioni,jijini Dar es salaam.
Kiongozi
wa Msafara wa Wafanyabiara hao ambaye ni Waziri wa Masuala ya Kiuchumi
na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig akizungumza na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet
Kairuki.
Meneja wa
Kitengo cha Uratibu Miradi ya Ubia (Sekta ya Umma na Binafsi) wa
TIC,Said Amir akitoa ufafanuzi juu ya maswala ya ubia katika
miradi,wakati wa mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa
wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na
kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika
jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es
salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirika wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC),Revocatus Arbogust akichangia jambo katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (wa pili kushoto) akiongea na
ujumbe huo wakati akiwaonyesha moja ya Jengo lilalotumiwa Kituo hicho lililojengwa na Wajerumani.
No comments:
Post a Comment