Wasichana London wajiunga na IS Syria
Uturuki
imeshutumu Uingereza kwamba imechukua muda mrefu kuijulisha nchi hiyo
kuhusu wanafunzi wa kike watatu waliokuwa wakisoma London Uinger kwamba
walisafiri kwenda nchini Syria kwa lengo la kujiunga na Islamic State.
Inaelezwa
kuwa wanafunzi hao walipanda ndege ya shirika la ndege la Uturuki
kutoka Uingereza na walihitaji hati ya kusafiri na visa kuingia Uturuki.
Sakata la wanafunzi hao wa kike kutoka London kwenda kujiunga na
wapiganaji wa Islamic State limekuwa limeshtua wengi.
Huku
serikali ya Uturuki inasema ingechukua hatua kama ingepewa taarifa
mapema Naibu Waziri Mkuu wa Bulent Arinc anatupa lawama moja kwa moja
kwa Uingereza kwamba iliichelewa kuijulisha nchi hiyo kabla ya wanafunzi
hao hawajaingia katika mji mkuu wa Instanbul.
"Tumefuatilia
na tumezuia watu wapatao elfu kumi ambao hapo awali waliripotiwa kwetu
kutaka kuingia Uturuki kwa tuhuma za kutaka kuendesha shughuli za
kigaidi. Tumetimiza wajibu wetu. Kama Serikali ya Uingiereza
ingetujulisha mapema maafisa wetu wa usalama wangechukua hatua
madhubuti. Tunaamini kuna haja ya kuanganisha nguvu kwa pamoja ili
kuratibu na kupambana na ugaidi." Alisema.
Wakati
kukiwa na taarifa hizo za wanafunzi wa kike waliokuwa wakisoma London
Uingereza kuingia nchini Syria kujiunga na Islamic State
Nayo
serikali ya Ufaransa kwa mara ya kwanza imezikamata hati za kusafiria za
raia wapatao sita ambao wanatuhumiwa kwenda nchini Syria kujiunga na
wapiganaji hao wa Islamic State.
Waziri wa
Mambo ya ndani wa ufaransa Benard Cazeneuve amesema kitengo cha ujasusi
kinaamini kwamba watu hao walikuwa na mpango wa kusafiri na kwamba
swala hilo linahusiana na mambo ya usalama.
"Tunaamini
hatua hizi zilizochukuliwa zimefanikiwa kwa sababu kama raia wa
Ufaransa watakwenda kupigana Iraq na Syria watasababisha hatari kubwa
kwa usalama wa taifa wakati watakaporudi. Wanaweza kuendesha vitendo vya
kigaidi kwa kiwango kikubwa." Alisema.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment