TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, February 5, 2015

IVORY COAST YATINGA FAINALI AFCON 2015 


Kipa wa DRC, Kidiaba akijaribu kuokoa mpira wa kichwa ulipigwa na Gervinho bila mafanikio. Hata hivyo mpira huo uliokolewa na mchezaji wa DRC ukielekea nyavuni.
KIKOSI cha Ivory Coast kikiongozwa na nahodha wake, Yaya Toure kimefanikiwa kutinga katika fainali za michuano ya Afcon 2015 baada ya kuichapa DR Congo mabao 3-1 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa usiku huu Equitorial Guinea.
Wafungaji wa mabao ya Ivory Coast walikuwa Yaya 21', Gervinho 41', Kanon 68' huku bao la DR Congo likifungwa na Mbokani 24' kwa penalti.
Kwa matokeo ya usiku huu, Ivory Coast wanasubiri mshindi wa mechi ya kesho kati ya Ghana na Equitorial Guinea kucheza naye katika fainali itakayopigwa Februari 8, mwaka huu.
DR Congo wanasubiri atakayefungwa kwenye mechi ya kesho ili wacheze naye Februari 7, mwaka huu kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu na ya nne.Globalpublishers

No comments:

Post a Comment