TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, February 6, 2015

Afrika ibuni ushirikiano wa Ulinzi

Wajumbe katika mkutano maalumu wa Usalama wa Bara la Afrika wametoa wito kufanywe mabadiliko katika majeshi yote Barani. Maafisa katika mkutano huo walisema kuwa mbinu mpya zinapaswa kutumika ikiwa majeshi katika Bara la Afrika watakuwa na matumaini yo yote ya kukabiliana na vitisho vya Waislamu wenye itikadi kali na uhalifu wa kimataifa.
Mhariri wa BBC wa Masuala ya Afrika, Mary Harper alihudhuria mkutano huo maalumu uliofanywa jijini London.
Vikundi vya wapiganaji wa Kiislam wanaoendesha operesheni yao katika eneo la nusu duara kutoka mashariki hadi magharibi wamejizatiti kimapigano kwa kuwa na teknolojia ya juu kulinganisha na majeshi ya usalama ya serikali za mataifa hayo.BBC
Vifaru na magari ya deraya havina upinzani inapokuja kukumbia katika maeneo yasiyo na miundo mbinu mizuri ya barabara. Kushindwa kwa majeshi ya usalama ya Nigeria kuwatokomeza wapiganaji wa kundi la Boko Haram ni jambo la kuzingatiwa.
Mafanikio ya hivi karibuni dhidi ya kundi la Kiislam la Al Shabaab yamechangiwa na sehemu ya muundo wa mafunzo uliotolewa na Marekani kwa majeshi ya serikali ya Somalia, na kuimarika kwa masuala ya kiintelijensia kwa kutumia ndege zisizo na marubani kumesaidia kubaini maeneo ya kushambulia kwa manufaa. Meja Jenerali wa zamani wa jeshi la Nigeria Ishola Williams anaamini majeshi ya nje yatoke katika mataifa jirani.
"Tunakiwa kutofautisha kati ya Ufaransa nchini Mali na Chad nchini Nigeria. Ni majirani. Kama nyumba yao inaungua moto na jirani yako hakusaidii, moto utakuja katika nyumba yako pia. Kwa hiyo ni muhimu kwamba majirani wasaidiane. Wakati unakuja kutoka mbali-kilomita elfu nne - unakuwa pia mbali sana kuelewa moto huu unahusu nin I hasa na namna ya kuuzima."
Si makundi yenye misimamo mikali ya kidini peke yake ndiyo yanayoweza kusababisha vurugu. Hali ya kutoweka kwa amani na utulivu katika mataifa ya Afrika pia kunaweza kuwa ni ushirikiano kati ya wapiganaji wa Kiislam na magenge ya uhalifu yanayosafirisha silaha, madawa, watu, sigara, fedha na dawa bandia, Na kwa kuwa uhalifu hauna mipaka, wajumbe wamekubaliana njia pekee kupambana na makundi haya ni kwa ushirikiano zaidi wa kikanda kwa kuzingatia vigezo na masharti. Lakini imeonekana kwa ujumla viongozi wa Afrika kutiliana mashaka. Huenda isiwezekane kuruhusu majeshi yao kushirikiana kufanya kazi kwa uaminifu hivi karibun

No comments:

Post a Comment