Jordan yatekeleza mashambulizi dhidi ya IS
Ndege za kivita ziliyoendesha mashambulizi dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu
Na RFI
Serikali
ya Jordan imetangaza kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za
kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Islamic State baada ya kuahidi
kulipiza kisasi baada ya mauaji ya rubani wake wa kijeshi juma hili.
Duru za
Kijeshi za Jordan zinasema kuwa ndege kadhaa za kivita zililenga kambi
za Islamic State hapo jana hasa ile ya mafunzo ya vikundi hivyo vya
kigaidi pamoja na ghala za silaha na kusema kuwa baada ya maangamizi
hayo ndege zao zimerudi salama nyumbani.(P.T)
Aidha,
katika mashambulizi hayo, nchi ya Marekani imetoa msaada wa kijeshi wa
ndege aina ya F-16 na F-22 kwa ajili ya usalama wa ndege za Jordan
pamoja na msaada wa mafuta wamesema maofisa wa Marekani.
Leo
Ijumaa, maandamano yanatarajiwa kufanyika nchi nzima kuonyesha
mshikamano na familia ya rubani aliyeuawa kwa kuchomwa moto na ambapo
mfalme wa Jordan Abdullah II akiambatana na Waziri mkuu Abdullah Nsour,
alitembelea siku ya Alhamisi familia ya rubani huyo kwenye umbali wa
kilomita 120 kutoka Amman, ambapo hema kubwa imejengwa kupokea
rambirambi.
Tayari nchi ya Jordan imewaonya wanajihadi wawili wa Iraq waliokuwa wamepanga mashambulizi ya kigaidi katika nchi yao.
No comments:
Post a Comment