Kilichowapata wanafunzi hawa baada ya kuudhihaki utawala wa mfalme wao
Wanafunzi
 wawili nchini Thailand wamehukumiwa kukaa gerezani kwa muda wa miaka 
miwili na nusu kwa kosa la kuudhihaki utawala wa kifalme wa nchi hiyo 
kupitia mchezo wa jukwaani katika chuo kikuu cha Thammasat jijini Bankok.
Wanafunzi hao Patiwat Saraiyaem (23) na Porntip Mankong (26) walihukumiwa jana walipokutwa na hatia ya kutunha igizo walilolipa jina la ‘The Wolf Bridge‘ mwaka jana ambapo wasaidizi wa mfalme walisema imeudhihaki utawala wake.
Awali wanafunzi hao walihukumiwa kifungo
 cha miaka mitano kila mmoja lakini walipunguziwa hadi miaka miwili na 
nusu baada ya kukiri kosa.

“Mahakama
 ijejiridhisha kuwa ushiriki wao katika mchezo wa jukwaani 
umeudhalilisha utawala wa kifalme, lakini baada ya kuirahisishia 
mahakama kwa kukiri kosa tuliamua kuwaounguzia kifungo“alisema Jaji wa Mahakama.
Inasemekana sababuza kutunga igizo hilo 
ni kusherehekea miaka 40 ya wanafunzi wachuo hicho kupigwa na wanajeshi 
wa Taifa hilo mwaka 1973 walipoandamana kudai demokrasia.

No comments:
Post a Comment