TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, February 27, 2015

Washtakiwa CUF wawazidi ujanja polisi

lipumba
Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam
HATI ya kuwafutia mashtaka wafuasi 30 wa Chama cha Wananchi (CUF) waliotakiwa kuunganishwa katika kesi moja na Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, imezua sintofahamu baada ya wafuasi hao kutoweka.

Wafuasi hao waliotakiwa kuachiwa na kukamatwa tena walitoweka jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru, baada ya kukubali maombi ya kuwaachia huru yaliyowasilishwa na DPP.

DPP aliwasilisha hati ya kuomba washtakiwa hao waachiwe huru (nolle prosequi) kwa madai kwamba Jamhuri haina nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.

Hati hiyo iliwasilishwa chini ya kifungu cha sheria ya makosa ya jinai namba 91(1) na mahakama ilikubali kuwaachia huru.

Jamhuri iliomba kufanya hivyo kwa lengo la kuwaunganisha katika kesi moja na Profesa Lipumba, lakini hawakuweza kufanya hivyo kwa sababu washtakiwa mara baada ya kuachiwa hawakukamatwa tena, walitoweka katika eneo la mahakama bila kusubiri usafiri wa mabasi wanayotumia kila wanapofika hapo.

Wakati watuhumiwa hao wameshatoweka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, aliiomba mahakama kumbadilishia hati ya mashtaka Profesa Lipumba kwa kuwaongeza washtakiwa wengine 30.

Kweka alipokuwa akiwasilisha hoja hiyo, tayari washtakiwa hao walishatoweka katika eneo la mahakama, aliyebakia ni Profesa Lipumba na wafuasi wengine wa kawaida waliofika kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo, Wakili Peter Kibatala anayemtetea Profesa Lipumba, alipinga kubadilishwa kwa hati hiyo, akidai waliwasilisha pingamizi la awali dhidi ya mashtaka hayo.

Kibatala alidai miongoni mwa hoja za pingamizi ni kuhusu uhalali wa hati ya mashtaka na mamlaka ya mahakama kusikiliza kesi hiyo.

Alidai kutokana na mapingamizi hayo, mahakama haiwezi kukubali kubadilisha hati hiyo ya mashtaka.

Hata hivyo, Kweka alidai mabadiliko ya hati hiyo ni kuwaongeza washtakiwa na si kubadili kitu kingine chochote.

Hakimu alikubali kumuunganisha Profesa Lipumba na wenzake 30 ambao hawakuwapo mahakamani na Jamhuri waliomba hati ya wito kwa washtakiwa walitoweka ili wafike mahakamani Machi 23, mwaka huu.

Washtakiwa walioachiwa huru na kutoweka ni Shaabani Ngurangwa, Shabani Tano, Shabani Abdallah, Juma Mattar, Mohammed Kirungi, Athumani Ngumwai, Shweji Mohammed, Abdul Juma, Hassan Saidi, Hemed Joho, Mohammed Mbaruku na Issa Hassan.

Wengine ni Allan Ally, Kaisi Kaisi, Abdina Abdina, Allawi Msenga, Mohammed Mtutuma, Salehe Ally, Abel Hatibu, Bakari Malya, Abadallah Ally, Said Mohammed, Salimu Mwafisi, Salehe Rashid, Abdallah Said, Rehema Kawambwa, Salma Nduva, Athumani Said, Dickson Leason na Nurdin Msati.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani Januari 29, mwaka huu wakikabiliwa na mashtaka matatu. Inadaiwa Januari 27, mwaka huu, katika ofisi ya CUF Temeke Hospitali, walikula njama, walikusanyika isivyo halali kwa nia ya kuandamana kwenda Mbagala.

Katika shtaka la tatu washtakiwa wanadaiwa siku hiyo ya tukio waligoma baada ya kutolewa makatazo halali maeneo ya Mtoni Mtongani walipokuwa wamekusanyika.
Profesa Ibrahim Lipumba katika hati yake ya mashtaka anadaiwa Januari 22 na 27, katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam aliwashawishi wafuasi wake kutenda makosa hayo ya jinai.CHANZO:MWANANCHI

Aveva: Sina mpango wa kujiuzulu Simba 

simba3
Dar es Salaam. Wakati kuna madai ya mpasuko wa uongozi, ukata mkubwa na madeni kwenye klabu ya Simba, rais wa klabu hiyo Evance Aveva amesema ajiuzulu, wanaotaka afanye hivyo wafuate taratibu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Aveva alisema kuwa kuna vyombo rasmi ambavyo vinafanya kazi ndani ya klabu hiyo zikiwamo kamati za kisheria, kamati ya mashindano, kamati ya utendaji na kwamba kama kuna tatizo wanachama wanajua taratibu za kufuata.
"Matokeo ya mpira ni hali ya mchezo, tumewapa wachezaji kila kitu, hakuna mchezaji anayedai zaidi ya posho yao ya muda ya mchezo wao na JKT Ruvu, Sh600,000 na kule Shinyanga viongozi wote tulikwenda na kuna motisha walipewa, sasa kosa letu viongozi ni lipi?"alihoji
"Mkutano mkuu wa wanachama upo pale pale, utafanyika Machi Mosi, wanachama walio hai wajitokeze kwa wingi pale Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam,"alisema.
Alieleza kuwa hakuna tofauti kati yake namakamu wake, Geoffrey Nyange 'Kaburu' ambaye inadaiwa kamati ya utendaji ya klabu hiyo imempiga marufuku kujihusisha na masuala ya timu.
Kumekuwa na madai kuwa Kaburu amezuiwa kwa kile kwa kuwa amekuwa akimwingilia kocha (Goran) majukumu yake ikiwa ni pamoja na kugawa wachezaji.
"Madai hayo Kaburu tulimuuliza akakataa, hatuna ugomvi wowote naye, ni kiongozi mwenzetu na tunaelewana vizuri na muda si mrefu nimetoka kuzungumza naye kwa simu, alichaguliwa na wanachama kama mimi, hatujafikia hatua ya kusimamishana, viongozi wote tupo kitu kimoja,"alisema.
Kwa upande wake, Kaburu hakupatikana jana kuzungumzia mgogoro wake na viongozi wenzake licha ya kutafutwa kwa muda mrefu.CHANZO:MWANANCHI

Tibaijuka abishana dakika 415, Chenge aenda Mahakama Kuu 


Dar es Salaam. Wakati Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka jana alitumia dakika 415 (takribani saa 7) akibishana katika mpambano mkali wa kisheria kuhusika kwake katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, mwenzake wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge aliamua kutimkia Mahakama Kuu kukwepa kuhojiwa na Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Jana, mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Hamisi Msumi alitoa uamuzi kuhusu pingamizi la Chenge aliyetaka baraza hilo lisisikilize shtaka lake la kukiuka maadili ya uongozi wa umma.
Hata hivyo, Chenge alikwamisha kwa mara ya pili baada ya kuomba kwenda Mahakama Kuu kutafuta tafsiri iwapo baraza hilo linaweza kusikiliza shauri lake kinyume na amri ya mahakama iliyoagiza lisijadilie na taasisi kwa kuwa kuna kesi kadhaa mahakamani zinazohusiana nalo.
Profesa Tibaijuka na Chenge kila mmoja aliingiziwa Sh1.6 bilioni kwenye akaunti zao binafsi kutoka kwa mkurugenzi wa VIP Engineering iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa za kampuni ya Independent Power Solution Limited (IPTL).
Baraza hilo, linasikiliza mashauri hayo kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 katika vipengele vya matumizi mabaya ya madaraka na sakata la escrow.
Chenge, juzi katika baraza hilo alipoitwa kuhojiwa aliibua hoja ya zuio la Mahakama Kuu na baada ya mabishano ya kisheria, Jaji Msumi alisema angekwenda kuisoma amri huyo kisha kutoa uamuzi wake jana.
Akisoma uamuzi huo, Jaji Msumi alisema: "Mlalamikiwa ametoa hoja ya amri ya Mahakama Kuu kuwa ndiyo hiki kinachojadiliwa, chimbuko lake ni miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow ambalo chimbuko lake ni bungeni na mahakama ilizuia lakini amri hiyo haizuii mamlaka hii."
"Orodha ya taasisi zilizotajwa hailihusu baraza hili, wadaiwa wote pamoja na mawakala, watumishi, wasaidizi wao au watu wengine wanaofanya hili. Amri iliyoandikwa, Baraza si mlengwa wa hili. Kinachozuiwa kufanywa ni kupelekwa bungeni au kujadiliwa taarifa ya (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pamoja na umiliki wa IPTL," alisema.
Akihitimisha kusoma uamuzi wa baraza hilo, Jaji Msumi alisema: "Hoja iliyotolewa na mlalamikiwa haina msingi na tunaomba kuendelea kulisikiliza."
Mara baada ya kumaliza, Chenge aliyekuwa amevalia shati la kitenge na suruali nyeusi akiwa haonyeshi kuwa na wasiwasi alisema: "Nashukuru kwa uamuzi huo lakini sina nia ya kubishana, natoa hoja ya kukata rufaa ya kwenda Mahakama Kuu ili mahakama itafasiri kama Baraza lina mamlaka ya kujadili suala hili."
Chenge ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema: "Kama wanasheria wa sekretarieti wangejituma kidogo kwenda masijala ya Mahakama Kuu kupitia wangeliona hili. Amri hii ya zuio ni pana kuliko uamuzi wa Baraza lako uliofikia, naomba nitumie nafasi hii kwenda Mahakama Kuu."
Akihitimisha hoja hiyo, Jaji Msumi alisema: "Nakuruhusu, niongeze tu sina hakika kama kanuni zimetengenezwa kuruhusu rufaa na kama hazipo kutakuwa na utaratibu. Ukipeleka itasaidia kujenga Baraza lakini Mahakama Kuu ina haki, kila mtu ana haki kwa suala lolote, mimi siwezi kukuzuia."Mara baada ya uamuzi huo, Chenge akiwa anatoka ukumbini waandishi wa habari walianza kumpiga picha huku wengine wakimtaka kuzungumzia uamuzi wake wa kupeleka suala hilo Mahakama Kuu, lakini yeye alisema: "Nani anataka nimpeleke tuisheni," kauli iliyowafanya waandishi hao kucheka.
Profesa Tibaijuka
Shauri la Profesa Tibaijuka lililoanza kusikilizwa saa 3:16 asubuhi hadi saa 5:18 asubuhi kabla ya kuahirishwa na kurejea tena saa 6.30 mchana hadi lilipohitimishwa saa 11.23 jioni, lilivuta hisia za wananchi na watumishi mbalimbali wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Barbro Johansso wakiongozwa na Mkuu wa Shule hiyo, Halima Kamote.
Mashtaka
Akisoma hati ya malalamiko dhidi ya mbunge huyo wa Muleba Kusini, mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili, Wemaeli Wilfred alisema: "Mheshimiwa Profesa Anna Tibaijuka kwa kutumia wadhifa wake (waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi) alishawishi na kuomba na kupokea fedha Sh1.617 bilioni kutoka kwa James Rugemalira.
Mara baada ya kumaliza kusoma hati hiyo, Wakili wa Profesa Tibaijuka, Rugemeleza Nshala alisimama na kusema: "Tunayakataa yote."
Kutokana na kauli hiyo, Jaji Msumi aliingilia kati na kusema: "Hii siyo mahakama ya kisheria, taratibu zetu siyo za kimahakama, hivyo ni vizuri kuyafikiria hayo."
Ushahidi
Baada ya kauli hiyo shahidi wa Sekretarieti, Waziri Kipacha ambaye pia ni Katibu Msaidizi, Idara ya Siasa ya Sekretarieti alisimama na kuanza kutoa ushahidi wake akiongozwa na Wilfred.
Shahidi huyo alisema alichokifanya Profesa Tibaijuka (kuomba na kupokea fedha hizo) wakati huo akiwa waziri, ni kinyume na sheria za maadili ya vingozi wa umma.
"Kuna tatizo, kwa mujibu wa masharti ya maadili ya viongozi wa umma hawaruhusiwi kuomba maslahi ya kiuchumi kutoka kwa mtu yeyote, mheshimiwa Tibaijuka Februari 12 mwaka 2014 alipokea fedha kutoka VIP Sh1.617 bilioni...hapa kuna tatizo la kimaadili."
Kipacha aliendelea kulieleza baraza hilo kuwa: "Kiongozi wa umma haruhusiwi kupokea maslahi ya kiuchumi lakini mheshimiwa Tibaijuka alifanya hivyo akijua kuwa ni makosa kutokana na sheria ya maadili ya viongozi wa umma."Profesa Tibaijuka kupokea kiasi kikubwa cha fedha kama hicho na wadhifa aliokuwa nao wa uwaziri ni ukiukwaji wa sheria za viongozi wa umma mheshimiwa mwenyekiti. Viongozi wa umma wanapaswa kuzingatia maadili wanapokuwa na uhusiano na kampuni au taasisi binafsi."
Baada ya maelezo hayo, Wakili Nshala alimuuliza Kipacha kuwa ni kosa gani alilolifanya kupokea mchango wa shule kama alivyokwishaeleza?
Kipacha alijibu: "Hapa ni ukiukwaji wa sheria ya maadili, Profesa Tibaijuka alipokea mchango ambao ni kiasi kikubwa cha fedha tena kwa kupitia akaunti yake binafsi, jambo ambalo ni kinyume kabisa cha sheria hii."
Nshala aliuliza tena: "Je, kama kiongozi wa nchi yetu ana jukumu la kuhamasisha na kusaidia watoto wetu kupata elimu, sasa hapa Profesa Tibaijuka kosa lake ni lipi?
Kipacha alijibu: "Kama kusaidia kwa kutoa fedha zake mfukoni siyo kosa na kama unachangisha au kuhamasisha watu kuchangia elimu na fedha hizo zinakwenda moja kwa moja kwa walengwa siyo kosa, lakini fedha hizo zikiingia moja kwa moja kwako hapo ni makosa kwa mujibu wa sheria hii ya maadili ya viongozi wa umma."
Nshala aliendelea kumuuliza, "Baada ya kufuatilia ninyi kwa uchunguzi wenu baada ya yeye (Profesa Tibaijuka) kuingiziwa fedha mlibaini nini?"
Kipacha kwa upole na kujiamini wakati wote alijibu: "Tulibaini fedha hizo zilianza kutoka kwa mafungu. Februari 18, 2014 zilitoka Sh1 bilioni kwenda Bank M na Machi 12, 2014 zilitoka Sh500 milioni kwenda Bank M na kubakiwa na Sh117 milioni katika akaunti yake ambayo hatujui alizifanyia nini. Lakini mwenyekiti hapa lalamiko ni ukiukwaji wa maadili tu."
Nshala aliuliza tena: "Kwa nini katika uchunguzi wenu hamkwenda kuwahoji Bank M au bodi ya wadhamini wa shule kwa kuwa ndiko fedha zilikwenda na iwapo wao walitoa uamuzi huo?
Kipacha alisema: "Kwa mujibu wa sheria hii sisi hatukuona sababu ya kwenda kuwahoji wao."
Baada ya kauli hiyo, Jaji Msumi aliingilia kati na kusema: "Katika uchunguzi wenu kwa nini hamkwenda kuhoji zaidi wakati mnasema kuna taasisi imenufaika kwa nini hamkwenda huko?
Akijibu hoja hiyo, Kipacha alisisitiza kuwa hawakuona sababu ya kufanya hivyo.
Sh10 milioni za mbogaHoja iliyoibua vicheko barazani ni kauli ya Profesa Tibaijuka kuwa kati ya fedha hizo alichota kwanza Sh10 milioni za kununua mboga.
Akitoa utetezi wake ambao mara zote ulikuwa ukiwafanya watu waliojaa ukumbini humo kuangua vicheko, Profesa Tibaijuka akihojiwa na mwanasheria wa sekretarieti hiyo, Getiruda Cyriacus aliyetaka kujua kama fedha hizo ziliingia Februari 12, 2014 kwa nini zilitoka Februari 18, mwaka huo na wakati huo huo kuna kiasi cha Sh10 milioni kilitoka mapema?
Profesa Tibaijuka alisema: "Nilitoa kiasi hicho kwenda kununua mboga, kwani kuna kosa gani."
Akiendelea, Profesa Tibaijuka alisema: "Uongozi mzima wa shule ya Babro wanafanya kazi kwa uadilifu, uwazi na ukweli wa hali ya juu na mimi kuomba mchango wa kuwasaidia watoto wa kike waliokuwa hawana fursa ya kupata elimu bora sioni kosa lake.
"Harakati hizi zitaendelea kwani nimekuwa nikizifanya nje na ndani ya nchi na ndiyo maana Rais mstaafu, Benjamini Mkapa alitupa kiwanja cha shule hiyo inayopigiwa kelele na yeye alishachangia fedha na watu wengine wakiwamo wafadhili wakubwa, mfano Serikali ya Sweden iliyochangia zaidi ya Sh8 bilioni lakini leo hii Sh1.6 inanidhalilisha hapa."
Aliongeza: "Mimi ni mstaafu wa Umoja wa Mataifa nina mafao yangu napata na nina akaunti za benki kama 10 ndani na nje ya nchi, sasa hii ya Rugemalira kama ningetaka angeiingizia katika akaunti nyingine, lakini yeye alisema ili asaidie shule nifungue akaunti Benki ya Mkombozi, sasa ningefanyaje?
Profesa Tibaijuka aliongeza, "Leo hii nadhalilishwa na kusimamishwa hapa kwa harakati zangu za kumkomboa mtoto wa kike, niwahakikishie kuwa nitaendeleza harakati hizi na malengo yangu ni kuhakikisha kila kanda kunakuwa na shule hizi za mfano, tulianza na Dar es Salaam, Bukoba sasa tunatafuta kiwanja Mwanza na Mbeya."
Mbunge huyo aliambatana na mashahidi wake wawili, Balozi Paul Rupia ambaye ni mlezi wa Bodi ya Wadhamini wa shule hiyo na mwenyekiti wa bodi hiyo, Simon Odunga ambao wote kwa pamoja walisema fedha walizopokea kutoka kwa Rugemalira kupitia akaunti ya Profesa Tibaijuka zilitumika kulipa deni la Sh2 bilioni walilokuwa wakidaiwa na Bank M, ambalo hata hivyo halikumalizika.
Baada ya utetezi huo, Jaji Msumi alizitaka pande zote ziandae majumuisho ambayo yatawasilishwa kabla ya Machi 13 mwaka huu, ili Baraza liandae mapendekezo ya siri yatakayopelekwa kwenye mamlaka za juu.CHANZO:MWANANCHI

KIKWAZO CHA UKAWA KUSIMAMISHA MGOMBEA MMOJA WA URAIS

Stori: mwandishi wetu
PRESHA inazidi kuongezeka kila kukicha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2015 ambapo sarakasi mbalimbali za kisiasa zinaendelea kuchezwa na wafuasi wa vyama vyote bila kujali chama tawala au vyama vya upinzani.
Uwazi Mizengwe limebaini kuwa macho na masikio ya wengi, yameelekezwa kwenye muungano wa vyama vinne vya kisiasa vya upinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), NCCR Mageuzi na NLD vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
WANANCHI WANASEMAJE?
Uwazi Mizengwe liliingia mitaani kujaribu kutafuta mawazo ya wengi.
"Ni dhahiri kwamba suala la Ukawa kumsimamisha mgombea mmoja haliwezekani, lazima dakika za mwisho Ukawa watavurugana," alisema Saleh Kiwia, mkazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Uwazi halikuishia hapo, liliendelea kudodosa huku na kule na kubaini kuwa suala la Ukawa kumsimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais, ni gumu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo nguvu iliyonazo chama kimojakimoja, wafuasi na ushawishi kwa wananchi.
"Kwa ushawishi na nguvu ilizonazo Chadema, haitakuwa rais kwa chama kingine kumsimamisha mgombea upande wa Bara wakati tayari wapo Freeman Mbowe na Dokta Wilbroad Slaa ambao wana ushawishi mkubwa miongoni mwa wapiga kura," alisema msomaji mwingine kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini.
LIPUMBA TAYARI AMESHATANGAZA NIA
Wakati vuguvugu hilo likiendelea, hivi karibuni CUF kiliitisha mkutano na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine, kilimtangaza mwenyekiti wake wa taifa, Ibrahim Lipumba kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo, alinukuliwa akisema: "Kwa upande wangu mie kama mkurugenzi wa uchaguzi nina imani na Profesa Lipumba, kuwa hatakuwa ndiye mgombea wetu wa urais tu kwa CUF bali hata kwa upande wa Ukawa,"alisema Mketo.
Kauli hiyo ilipokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa wafuasi wa vyama hivyo vya siasa, kila mmoja akizungumza lake."Haiwezekani Lipumba ndiyo awe mgombea wa Ukawa kwa sababu Chadema ndiyo chenye nguvu upande wa Bara," alikaririwa Dickson Mapunda, mfanyabiashara wa Soko la Kariakoo.
MASHARTI YA CHADEMA KWA VYAMA VINGINE
Duru nyingine za kisiasa kutoka ndani ya Chadema, zinaeleza kwamba chama hicho hakiwezi kukubali kuona mgombea kutoka chama kingine anasimama kuwania nafasi ya urais kwa sababu chenyewe ndiyo chenye nguvu, mtandao mpana na wafuasi wengi kwa hiyo ni lazima kitoe mgombea.

"Masharti makubwa ya Chadema kwa vyama vingine ni kwamba lazima vikubaliane kumuunga mkono mgombea atakayetoka kwenye chama hicho, jambo ambalo halitakuwa rahisi kwa sababu tayari CUF wameshaonesha wanataka nani ndiyo awe mgombea, lazima watavurugana tu," alikaririwa Mwanaisha Mataka, mkazi wa Kinondoni.CHANZO:Globalpublishers

Tuesday, February 24, 2015

Wasichana London wajiunga na IS Syria


Uturuki imeshutumu Uingereza kwamba imechukua muda mrefu kuijulisha nchi hiyo kuhusu wanafunzi wa kike watatu waliokuwa wakisoma London Uinger kwamba walisafiri kwenda nchini Syria kwa lengo la kujiunga na Islamic State.
Inaelezwa kuwa wanafunzi hao walipanda ndege ya shirika la ndege la Uturuki kutoka Uingereza na walihitaji hati ya kusafiri na visa kuingia Uturuki. Sakata la wanafunzi hao wa kike kutoka London kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State limekuwa limeshtua wengi.
Huku serikali ya Uturuki inasema ingechukua hatua kama ingepewa taarifa mapema Naibu Waziri Mkuu wa Bulent Arinc anatupa lawama moja kwa moja kwa Uingereza kwamba iliichelewa kuijulisha nchi hiyo kabla ya wanafunzi hao hawajaingia katika mji mkuu wa Instanbul.
"Tumefuatilia na tumezuia watu wapatao elfu kumi ambao hapo awali waliripotiwa kwetu kutaka kuingia Uturuki kwa tuhuma za kutaka kuendesha shughuli za kigaidi. Tumetimiza wajibu wetu. Kama Serikali ya Uingiereza ingetujulisha mapema maafisa wetu wa usalama wangechukua hatua madhubuti. Tunaamini kuna haja ya kuanganisha nguvu kwa pamoja ili kuratibu na kupambana na ugaidi." Alisema.
Wakati kukiwa na taarifa hizo za wanafunzi wa kike waliokuwa wakisoma London Uingereza kuingia nchini Syria kujiunga na Islamic State
Nayo serikali ya Ufaransa kwa mara ya kwanza imezikamata hati za kusafiria za raia wapatao sita ambao wanatuhumiwa kwenda nchini Syria kujiunga na wapiganaji hao wa Islamic State.
Waziri wa Mambo ya ndani wa ufaransa Benard Cazeneuve amesema kitengo cha ujasusi kinaamini kwamba watu hao walikuwa na mpango wa kusafiri na kwamba swala hilo linahusiana na mambo ya usalama.
"Tunaamini hatua hizi zilizochukuliwa zimefanikiwa kwa sababu kama raia wa Ufaransa watakwenda kupigana Iraq na Syria watasababisha hatari kubwa kwa usalama wa taifa wakati watakaporudi. Wanaweza kuendesha vitendo vya kigaidi kwa kiwango kikubwa." Alisema.CHANZO:BBC

Raia sita wa Ufaransa wanyang'anywa pasipoti 

Mpiganaji wa Dola la Kiislam akishikilia bendera nyeusi ya Dola la Kiislam katika mji wa Racca (Syria) Juni 29 mwaka 2014.
Uamzi huo umechukuliwa na kutangazwa na wizara ya ya mambo ya ndani, ambayo imethibitisha kwamba watu hao sita wamekua wakijiandaa kusafiri kutoka Ufaransa kuelekea Syria.
Uamzi huo unaendana sambamba na sheria dhidi ya ugaidi iliyopitishwa mwaka 2014.
Uamzi uliyochukuliwa na wizara ya mambo ya ndani dhidi ya watu hao sita inapiga marufuku watu hao kusafiri nje ya Ufaransa. Utaratibu huu unaendana na sheria iliyopitishwa Novemba mwaka 2014, ambayo inapiga marufuku raia wa Ufaransa kusafiri kwenda Syria.
Ni wiki moja sasa, Waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, alitoa takwimu ya kuvutia, ambayo inaeleza kuwa idadi kubwa ya raia wa Ufaransa wamejiunga na makundi ya kijihadi. kwa mujibu wa Waziri mkuu, karibu raia 1400 wa Ufaransa wamekua na mawasiliano na makundi ya wanajihadi ambayo yanahusika na kuwaajiri na kuwapeleka watu katika makundi hayo kijihadi hususan kundi la Dola la Kiislamu linaolodhibiti baadhi ya maeneo ya Syria na Iraq.
Watu hao sita wana umri uliyo kati ya 23 na 28, na ni wakazi wa eneo la kusini mashariki mwa Ufaransa. Baadhi yao walishajielekeza nchini Syria katika miaka iliyopita.
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani, watu hao sita, ikiwa ni pamoja na wanaume na wanawake wamekua wakijiandaa kusafiri ili kujiunga na kundi la wanamgambo wa Dola la Kiislamu.CHANZO:R.F.I

Roboti yahudhuria masomo kama mwanafunzi 


Mwanafunzi mmoja katika mji wa Pennsylvania nchini Marekani alipata ajali ya gari na kuumia vibaya na sasa anahudhuria masomo kwa msaada wa njia ya roboti.
Cole Fritz alikuwa alikuwa hawezi kuhudhuria masomo yake mara baada ya ajali mwezi mmoja uliopita,lakini kwa sasa anaouwezo wa kufuatilia kila kinachoendelea kwa msaada wa roboti.
Pennsylvania ilikodisha kifaa hicho kutoka katika kampuni inayotoa mafunzo ya namna ya kutumia roboti hizo katika mitandao ya kijamii.Kimsingi kifaa hicho ni sawa na iPad ambayo imeinuliwa juu vya kutosha.Naye Cole huwa anakiendesha kifaa hicho kupitia kinakilishi chake na vitufe vya kubofyea kitu ambacho yeye anakielezea kuwa sawa na kifaa cha michezo ya kinakilishi ya runinga.ana sema Roboti hiyo inamsaidia kufuatilia masomo yake bila taabu yoyote na pia awapo shuleni anakutana na marafiki zake .
Ni vyema na furaha kubwa kuonana na kila mmoja niliye mzoea na kuzungumza nao.
Wakuu wa shule anakosoma Cole wanasema roboti hiyo inawasaidia kupunguza gharama za mwanafunzi huyo.na wanajaribu kuzungumza kuwa hawajui ingekuwaje kwa mwanafunzi huyo bila kifaa hicho,pengine ingewalazimu kumpeleka mwalimu kila siku nyumbani kwa akina Cole kumfundisha,lakini roboti hiyo inamsaidia Cole kupata elimu bora,kwa kumpa maelekezo kupitia waalimu wake kama kawaida na roboti hiyo imekuwa sehemu ya darasa la Cole.
Kwa muujibu wa maelezo ya Cole, roboti hiyo si sanifu sana lakini si haba ni mwanzo mzuri na maendeleo yako wazi mbele yake.
Madaktari wanaofuatilia afya ya kijana huyo ,wanasema kwamba Cole atarejea shuleni akiwa hali ya kawaida mapema mwezi ujao.CHANZO:BBC

Misri si mwenyeji wa AFCON 2017 


waziri wa michezo nchini Egypt Khaled Abdel-Aziz amethibitisha kuwa nchi yake imetupilia mbali jitihada zake za kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017.
Anasema,tumeamua kujiondoa kwenye maombi hayo na tutawaunga mkono Algeria.
Nchi za Gabon na Ghana ziliomba zabuni hiyo ,nalo shirikisho la soka barani Africa litatoa jina la mwenyeji wa michuano hiyo mnamo tarehe 8 ya mwezi April.
Libya nayo ilikuwa na tamanio la kuwa mwenyeji wa fainali za michuano hiyo lakini ilijiondoa kutokana na hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo.
Waziri Abdel-Aziz hakufunguka zaidi kueleza sababu za ziada za kujiondoa lakini imeshikilia msimamo huo baada ya mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA ,Hany Abu Rida kusema kwamba haina maana yoyote kwa nchi mbili za kiarabu kushindania zabunia hiyo.
Anasema Egypt haitaweza kushindana na Algeria lakini tuna hakikisha kutoa usaidizi makini kadiri tuwezavyo anahakikisha Abu Rida katika maelezo yake.
Kujiondoa huko kunakuja baada ya vifo vya mashabiki 22 mnamo tarehe 8 February wakati polisi na washabiki walipovaana kabla ya mchezo baina ya timu ya Zamalek ya Cairo na ENPPI.
Kufuatia tukio hilo shughuli zote za soka za ndani zimesimamishwa mpaka hapo itakapotangazwa tena lakini waziri mkuu wa Misri Ibrahim Mahlab anaamini kuwa ligi ya nchi hiyo haitaishia kufutwa ingawa kwa sasa tunaangalia zaidi suala la usalama michezoni na kupisha hali mbaya ya hewa iliyotokea michezoni.
Waziri huyo ametoa ahadi ya kujadili suala hilo wiki ijayo na kutilia mkazo vipaumbele vya mazungumzo hayo kuwa ni kuweka mambo katika mizania na hasa ligi kurejeshwa tena na suala la usalama wa wanamichezo.
Na kama Ligi itaendelea basi washabiki hawatahitajika uwanjani Mahlab ameelezea msimamo wa nchi yake.
Tukio hilo la hivi karibuni lililotokea katika mzunguuko wa kwanza wa ligi nchini humo,ambalo linakuja na amri ya kutoruhusu mashabiki uwanjani ili kunusuru usalama mchezoni,ikumbukwe kwamba tangu February mwaka 2012 mashabiki walipigwa marufuku kushuhudia mechi zikipigwa uwanjani kutokana na washabiki takribani sabini na wawili wa Al Ahly walipovaana na mashabiki wa timu ya Al Masry katika uwanja wa Port Said na kusababisha maafa hayo.CHANZO:BBC

SERIKALI YAPATA SH. BILIONI 15 ZA KULIPA MADENI YA MAHINDI 

SERIKALI Serikali imepata mkopo wa sh. bilioni 15 ambazo zitatumika kulipa kiasi cha madeni ya mazao ya nafaka ambayo wakulima wanaidai kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Iringa akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo katika mkoa huo.
Akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo (SACCOS) cha Mazombe kilichopo Ilula wilayani Kilolo, mwishoni mwa wiki, Waziri Mkuu alisema katika kipindi cha mwezi huu, Serikali imepata mkopo huo kutoka benki ya CRDB ambazo zimesambazwa kwenye mikoa mbalimbali ili kuwalipa wakulima hao.
Alisema hadi kufikia Machi mwaka huu, Serikali itahakikisha inamaliza kulipa madeni kwa wakulima ambao waliuza mazao yao kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).
Akifafanua kuhusu mgao wa fedha hizo, Waziri Mkuu alisema kanda ya Arusha wamepata sh. bilioni 1.72/-; kanda ya Dodoma sh. bilioni 2.02/-; kanda ya Kipawa sh. milioni 632.3/-; kanda ya Makambako sh. bilioni 4.58/-; kanda ya Shinyanga sh. milioni 238.85/-; kanda ya Songea sh. bilioni 1.97/- na kanda ya Sumbawanga sh. bilioni 3.82/-.
Alisema fedha hizo zimegawanywa kwenye vituo, vikundi na mawakala na kuongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika itatoa sh. bilioni 15 nyingine ili zigawanywe katika kanda na kumaliza kabisa madeni ya wakulima.
Alitoa ufafanuzi huo baada kutolewa malalamiko kuwa ucheleweshwaji wa malipo hayo kwa wakulima umewafanya baadhi yao washindwe kurejesha mikopo kwenye taasisi za fedha kwa wakati.
Alisema ucheleweshwaji wa malipo hayo ulitokana na ziada ya chakula kwenye msimu wa kilimo wa mwaka 2014 kuongezeka kwa kufikia zaidi ya tani milioni 1.3, ukilinganisha na ziada ya tani 300,000 za msimu uliopita. "Serikali ililazimika kununua mazao ya wakulima zaidi ya malengo yake... matokeo hayo mazuri ya kilimo, yalitokana na msisitizo wa Serikali kuwekeza kwenye pembejeo, mbegu bora pamoja na kuingiza nchini matrekta zaidi ya 1600.
Mapema, akisoma taarifa ya chama hicho mbele ya Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Mazombe SACCOS, Bw. Yohanes Mwemtsi, alisema kucheleweshwa kwa marejesho ya mikopo iliyochukuliwa na wakulima kunazorotesha maendeleo ya SACCOS hiyo kwa kushindwa kujiimarisha kimtaji.
Alisema licha ya changamoto hiyo, chama hicho kimeshatoa mikopo yenye thamani ya sh. bilioni 4.3 kwa wanachama wake zaidi ya 1,300 huku kukiwa na ongezeko la wanachama wapya kwa wastani wa asilimia 10 kila mwaka.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 23, 2015

Taarifa Rasmi ya Jeshi la Polisi Kuhusiana na Sakata la Kutekwa kwa Wanajeshi wa JKT Waliotaka kuandamana Kudai Ajira


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia vijana watano wa kundi la wahitimu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa tuhuma za kufanya uchochezi na kufanya mikusanyiko isiyo halali jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema vijana hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti kwa makosa ya kuunda kikundi kisicho halali kwa mujibu wa sheria za nchi na kuwahamasisha wenzao, kuandamana hadi Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete kudai ajira za kudumu.
 
“Tunawashikilia vijana watano ambao ndio viongozi wa kikundi kinachojiita umoja wa wahitimu wa Jeshi la Kujenga Taifa. Mwenyekiti ndio alikuwa wa kwanza kukamatwa na wengine tuliwakamata juzi mara baada ya kukusanyika eneo la Msimbazi Centre na Muhimbili,” alisema Kova.
 
Akieleza chanzo cha vijana hao kutaka kuandamana kuelekea Ikulu, alidai wahitimu hao wanadai kuahidiwa ajira za kudumu walipomaliza mafunzo yao na hivyo baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuajiriwa, ndipo wakaamua kuanzisha kikundi hicho ili kwenda kumwona Rais  Kikwete kumweleza tatizo la ajira linalowakabili.
 
“Vijana hawa wanadai kuwa waliahidiwa kupewa ajira za kudumu mara baada ya kumaliza mafunzo yao ya JKT.
 
" Jambo hili sio la kweli, kwani tumefanya uchunguzi na kubaini hakuna mkataba wowote unaosema wakimaliza mafunzo lazima waajiriwe, bali kila mtu anatakiwa kutumia ujuzi alioupata kujiajiri.  
 
"Lakini walipokaa kwa muda mrefu  bila kuona ahadi yao inatekelezwa, wakaamua kuanzisha kikundi chao ambacho sio halali kwa mujibu wa sheria za nchi.
 
"Hadi sasa tumeandaa jalada la mashitaka na tumelikabidhi kwa mwanasheria wa serikali kwa ajili ya kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hawa kujibu mashitaka yanayowakabili,” aliongeza Kova katika taarifa yake.
 
Alitaja vijana wanaoshikiliwa na Polisi kuwa ni Mwenyekiti wa kikundi hicho George Mgoba (28) mkazi wa Mabibo Loyola, Katibu wao Linus Emmanuel (28) mkazi wa Tabata, Emmanuel Richard (28) mkazi wa Kawe, Jacob Joseph (36) mkazi wa Mabibo na Rizione Ngowi (27) mkazi wa Mtoni Mtongani.
 
Akizungumzia tuhuma za kutekwa na kuteswa kwa George Mgoba, Kova alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini tukio hilo kama ni la kweli na kwanini watu hao walimteka.
 
 “Tunaendelea na uchunguzi kubaini kama ni kweli kijana huyo alitekwa kama anavyodai kuwa Februari 16 alitekwa na kupatikana tarehe 19 majira ya saa  nne usiku huko Tungi Kibaha kandokando ya barabara, pia tujue ni akina nani walimteka na kwasababu zipi kisha watu hao tutawapeleka mahakamani,” alisema Kova.
 
Kova alieleza kuwa “Februari 22 mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni, George Mgoba alijaribu kutoroka wadini katika Hospitali ya Muhimbili lakini polisi walibaini ujanja wake na kufanikiwa kumweka kizuizini. Lengo lake ilikuwa ni kukimbia matibabu na kuzua hofu kwa wananchi”.
 
Kwa sasa Mwenyekiti huyo wa vijana hao bado amelazwa katika  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akipatiwa matibabu. 
 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja katika Hospitali  hiyo ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha  alisema jana kuwa hali ya mtu huyo, inaendelea vizuri na afya yake imeimarika.
 
Wakati huo huo, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari baadaye jana, Kova alimtaka Makamu Mwenyekiti wa Vijana hao, Parali Kiwango (25) mkazi wa Temeke Mikoroshini ajisalimishe mara moja Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi, kabla jeshi hilo halijaanza kumtafuta.
 
“Jeshi la Polisi linamtaka Makamu Mwenyekiti ajisalimishe mara moja kwani jana alipoona Katibu wake amekamatwa alikimbia na kutokomea kusikojulikana. 
 
"Yeye kama ni mhitimu wa JKT hatakiwi kukimbia, bali ajisalimishe mwenyewe katika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Polisi Kanda  Maalumu Dar es Salaam au kituo chochote cha Polisi kilicho karibu na alipo,” aliongeza Kova.

Watanzania sasa Kupatiwa Viza Huko Huko India 


Wasafiri kutoka Tanzania kwenda India kwa  shughuli za matibabu na biashara wataruhusiwa  kupata visa wafikapo nchini humo.

Hayo yalisemwa na Balozi wa India nchini, Debnath Shaw wakati akijibu maswali ya wafanyabiashara wa kitanzania wakati wa mkutano baina ya wafanyabiashara wa ndani na wenzao kutoka jimbo la Gujarat India.
 
Alisema: “Tutahakikisha tunafanya utaratibu huo na utaanza siku za usoni ili kupunguza usumbufu wanaoupata Watanzania waendao India”.
 
Kwa upande wake, Ofisa Mkuu Mtendaji wa Global  Investors Consultstion Center (GICC), Shainul Bhanji alisema kutokana na ripoti ya Benki ya Dunia Tanzania imeonekana kuwa ni nchi yenye mazingira mazuri ya biashara kwani ripoti inaonesha Tanzania inaendelea kushika nafasi nzuri ukilinganishwa na nchi jirani za Kenya na Uganda.
 
“Tanzania ilikuwa nafasi  ya 142 kati ya 180 kwa mwaka 2011 lakini sasa imepanda hadi nafasi ya 131  huku Kenya ikiwa katika nafasi ya 136 na Uganda nafasi ya 132,” alisema Bhanji.
 
Naye Rais wa Taasisi ya Wenye Viwanda toka Jimbo la Gujarat India Amit Patel alisema kwa sasa India ni nchi ya nne kwa ukubwa kwa nchi zinazofanyabiashara kwa Afrika na wana uhakika kuwa watafanyabiashara kuzidi China, Marekani na Ulaya.
 
Alisema Serikali ya India imeahidi kutoa mikopo ya masharti nafuu ya bilioni 6 mwaka huu kwa nchi za Afrika ili kuboresha miundombinu na mazingira ya kufanyabiashara.
 
Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda nchini Francis Lukwaro alisema mkutano utasaidia wafanyabiashara wa Tanzania kujifunza mambo mapya ya kibiashara kutoka India.
 
Alisema kwa upande wa Tanzania kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara hawa kwani wengi wao ni wafanyabiashara wakubwa na wameendelea.

Radi Yaua Mwalimu na Wanafunzi 6 Kigoma


Watu saba wakiwamo wanafunzi sita wa darasa la nne katika shule ya msingi Nyakasanda na Mwalimu wa shule hiyo, Anderson Kibada wamekufa baada ya kupigwa na radi huku watu wengine 11 akiwemo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Laurence Sesegwa (42) wakijeruhiwa.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kigaga Daga alisema kuwa watu hao walifikwa na mauti hayo kufuatia mvua kubwa zilizonyesha zikiambatana na radi zilizoanza majira ya saa tano asubuhi zilizotokea katika kijiji cha Nyachenda wilaya ya Kasulu mkoani.
 
Mbali na Mwalimu Kibada aliyekufa hapo hapo, Mganga huyo Mkuu wa Wilaya aliwataja wanafunzi kuwa ni pamoja na Mary Steven (11), Severine Mussa (11) na Joseline Joseph (12). 
 
Aliwataja wanafunzi wengine waliofariki kuwa ni Joyness Simon (14), Nehemia Kepha (14) na Robin Gabriel (14).
 
Alisema kuwa hadi sasa wanafunzi wanne wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu ambao aliwataja kuwa Fadhila Emanuel (13), Matilda Moses (11), Bizimana Manjo (12) huku wanafunzi wengine saba wakiruhusiwa baada ya hali zao  kuwa nzuri.

Kilichowapata wanafunzi hawa baada ya kuudhihaki utawala wa mfalme wao

thai 
Wanafunzi wawili nchini Thailand wamehukumiwa kukaa gerezani kwa muda wa miaka miwili na nusu kwa kosa la kuudhihaki utawala wa kifalme wa nchi hiyo kupitia mchezo wa jukwaani katika chuo kikuu cha Thammasat jijini Bankok.
Wanafunzi hao Patiwat Saraiyaem (23) na Porntip Mankong (26) walihukumiwa jana walipokutwa na hatia ya kutunha igizo walilolipa jina la ‘The Wolf Bridge‘ mwaka jana ambapo wasaidizi wa mfalme walisema imeudhihaki utawala wake.
Awali wanafunzi hao walihukumiwa kifungo cha miaka mitano kila mmoja lakini walipunguziwa hadi miaka miwili na nusu baada ya kukiri kosa.
Thai King Bhumibol Adulyadej of Thailand surrounded by his family members
“Mahakama ijejiridhisha kuwa ushiriki wao katika mchezo wa jukwaani umeudhalilisha utawala wa kifalme, lakini baada ya kuirahisishia mahakama kwa kukiri kosa tuliamua kuwaounguzia kifungo“alisema Jaji wa Mahakama.
Inasemekana sababuza kutunga igizo hilo ni kusherehekea miaka 40 ya wanafunzi wachuo hicho kupigwa na wanajeshi wa Taifa hilo mwaka 1973 walipoandamana kudai demokrasia.

Taarifa kuhusiana na watoto zaidi ya 10 kufariki hospitali ya Amana

icu
Watoto zaidi ya 10 wamefariki dunia baada ya kukosa huduma ya joto katika hospitali ya Amana Jiji Dar es salaam.
Taarifa kutoka hospitalini hapo zinadai waliozaliwa kabla ya wakati  maarufu njiti walifariki dunia February 16 mwaka huu.
Chanzo cha vifo hicyo imetajwa kuwa ni uzembe wa wauguzi baada ya kukatika kwa umeme kwenye chumba walimohifadhiwa.
“Umeme ulikatika muda wa saa 5 asubuhi hadi saa 10 jioni ,wauguzi hawakutekeleza wajibu wao wa kuwaita wazazi wa watoto hao ili wawachukue kwa ajiliya kuwasaidia kupata joto, matokeo yake watoto walifariki dunia” anasema mmoja wa wazazi waliofiwa.
Hata hivyo baadhi ya madaktari wa hospitali hiyo waligoma kuzungumzia na Gazeti la JAMHURI kuhusu suala hilo huku mganga mkuu wa Hospitali hiyo  Dk. Meshack Shimwela akisema taarifa hizo si za kweli na huenda watoto hao walikufa kutokana na matizo menfine kwani wana jenereta za dharura

Rekodi hii inamfanya Cristiano Ronaldo kuingia kwenye list ya mashujaa wa Real Madrid

criiii
Neema imeendelea kubaki upande wa mshambuliaji Christiano Ronaldo baada ya juzi kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kumfanya kuwa mfungaji wa tatu kwa kuwa na magoli mengi katika historia ya soka la Hispania.
Katika mchezo wa juzi jumapili Ronaldo alihitimisha ushindi wao kwa kufunga goli la pili na kumfanya kufikisha jumla ya magoli 290.
Ronaldo ambaye pia mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or  ya mwanamichezo bora wa dunia kwa mara ya tatu ameshika nafasi hiyo akiwa amecheza michezo 289 huku nafasi ya pili ikishikwa na Alfredo Di Stefano ambaye amecheza michezo 392 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Raul Gonzalez mwenye idadi ya magoli 323 katika michezo 741.

Nchi kumi zilizotajwa kuwa sio salama kwa wanawake kutembelea wakiwa pekeyao

Russian-women-Beach-pictures-31
Yako mengi mazuri ya maeneo mbalimbali tunayajua, mfano ni ile list ya Majiji salama zaidi Duniani kwa kuishi, nikakuwekea na ile nyingine ya Beach kali zaidi duniani, leo nimeipata hii nashare na wewe tena mtu wangu.
Gazeti la Daily Mail ni moja ya Magazeti makubwa zaidi Uingereza na Ulaya, wataalamu wao wamefanya utafiti na kuyataja maeneo kumi ambayo siyo salama duniani kwa wanawake kutembelea kwa shughuli yoyote ikiwemo kutalii kama wakiwa peke yao.
  1. India: Jamaa wanasema huku kumekuwa na stori nyingi za matukio ya ubakaji wa wanawake, hii imefanya baadhi ya watalii kuwa na hofu ya kutembelea nchi hiyo. Ripoti hiyo inaonesha kunaripotiwa tukio la ubakaji kila ndani ya dakika ishirini.
  2. Brazil: Ripoti inaonesha matukio ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia, wizi wa kutumia silaha ni tatizo kwa nchi hii. Matukio ya ubakaji yameongezeka kwa 157% kati ya mwaka 2009 na 2012.
  3. Uturuki: Huku nako ishu ni matukio ya ubakaji, yanashika kasi kila siku.
  4. Thailand: Ishu kubwa ni unyanyasaji wa kijinsia kwa upande wa huku, dawa za kulevya na pombe zimetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa.
  5. Egypt: Tokea kumetokea mapinduzi ya utawala 2011 hali haiku sawa bado, unyanyasaji wa kijinsia nako umeshika kasi kubwa.
  6. Colombia: Ripoti hiyo inaonesha Polisi wanadili kwa kiasi kidogo sana na ishu ya kulinda wanawake, ni mara chache watuhumiwa wa makosa ya ubakaji wamefikishwa Mahakamani.
  7. South Africa: Hii ni ya kwanza kutajwa kutoka Africa, unyanyasaji wa kijinsia, wizi wa kutumia silaha, na ubakaji ni matatizo makubwa sana kwenye nchi hii.
  8. Morocco: Watalii wa kike wanashauriwa kuvaa kama wenyeji wa nchi hii lakini ishu za ubakaji zinatajwa kwa kiwango cha juu kwa watalii wanawake ambao wanakuwa peke yao.
  9. Mexico: Japo Serikali imeweka nguvu nyingi kuhakikisha tu watalii wanakuwa salama, bado wizi wa kutumia silaha uko kwa hali ya juu sana pamoja na ubakaji wa wanawake kwenye vyombo vya usafiri wengi imewatia hofu.
  10. Kenya: Utalii imekuwa biashara kubwa kwa nchi hii, ripoti hiyo imeitaja kuwa unyanyasaji wa kijinsia uko kwa kiwango kikubwa sana kwa wanawake.

Tuesday, February 17, 2015

'Magaidi wa Tanga' Watiwa Mbaroni.....Mwili wa Mwanajeshi wa JWTZ Aliyeuawa katika Mapigano hayo Waagwa 


Serikali imetoa taarifa rasmi kuhusu uhalifu uliotikisa mkoani Tanga, ikisema hali ni shwari na umma wa Watanzania upuuze taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikitia hofu.

Aidha, imesema  watu kadhaa wanashikiliwa wakihusishwa na uhalifu huo.
 
“Tunawashikilia ila mpaka sasa siwezi kukueleza idadi yao na kwamba ni wa kikundi cha ugaidi au la. Hao watu tunafanya nao mahojiano ili kuweza kuelewa kama wanahusika kwenye tukio hilo,”  alisema Kaimu Kamanda wa Polisi  wa Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki.
 
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Ndaki alisema hali katika kitongoji cha Majimoto, Amboni na mkoa wa Tanga kwa ujumla iko shwari. “Tunaendelea kufanya uchunguzi kubaini hao wahalifu pamoja na silaha zilizoibwa,” alisema.
 
“Tunaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano wao hasa wanapoona watu wenye majeraha au wanaowahisi kwamba ni wahalifu ili nasi tuweze kuwachunguza kama wanahusika kwenye tukio hili”, alisema.
 
Ingawa Kamanda hakuelezea mazingira ya kukamatwa kwa watuhumiwa, waandishi wa habari waliozuru eneo la Amboni  yalikotokea mapigano, waliarifiwa kwamba baadhi ya wavuvi kwenye Mto Zigi, walimkamata mtu wakimtuhumu kukutwa akifua nguo zenye damu.
 
Katika mapigano hayo baina ya askari na wahalifu, yalisababisha kifo cha askari wa JWTZ,  Sajenti Said Kajembe na wengine kujeruhiwa.
 
“Asubuhi wavuvi kadhaa walikuwa hapo mtoni ghafla walikutana na mtu pembeni ya mto akiwa anafua kanzu pamoja na vifaa fulani kama nguo za kufunika uso ..’maski’ ikabidi wawapigie haraka polisi simu lakini hawakuweza kupatikana na ndipo wakawapigia askari wa JWTZ ambao walifika haraka eneo la tukio na kumkamata mhusika”, alisema mkazi mmojawapo.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga,  Magalula Said Magalula aliwataka wakazi wa Tanga na vitongoji vyake, kuondoa hofu kwa kuhakikisha wanaendelea na shughuli zao za uzalishaji kwa sababu ulinzi umeimarishwa na hali ya usalama ni  shwari.
 
Pia, aliwataka wananchi na wageni wenye mpango wa kutembelea eneo la kihistoria la Mapango ya Amboni, kuendelea na ratiba zao kwa sababu eneo hilo liko salama na tangu awali halikuhusika kwenye vurugu hizo.
 
Magalula ambaye pia alikutana na waandishi wa habari, alisema “Hali ni nzuri ulinzi na usalama uko imara… naomba wananchi waondoe hofu, wawe na amani na waendelee na shughuli zao za uzalishaji… hakuna tatizo kabisa usalama umedhibitiwa vizuri.”
 
Mkuu huyo wa mkoa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, alisisitiza  “Naomba Watanzania wenzangu muelewe kwamba eneo lilipofanyika tukio la mapigano na wahalifu si pale yalipo mapango ya Amboni ... maeneo hayo yapo mbali na nitoe mwito kwa wageni wenye mpango wa kutembelea hapo wawe huru kufanya hivyo mahali hapo ni salama.”
 
“Naomba Watanzania nchini kote kwa ujumla wawe na amani kwa sababu Tanga iko shwari hakuna tena hizo vurugu za wahalifu… naomba wasiamini sana taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii… sisi tuko shwari na shughuli za kijamii zinaendelea kama kawaida ikiwemo Amboni,” alisema.
 
Akizungumzia mapigano hayo yaliyotokea  Februari 14,  alisema licha ya majibizano ya kurushiana risasi yaliyofanywa na askari wa Polisi kwa kushirikiana na wa JWTZ , uchunguzi unaendelea  kuwapata wahusika.
 
“Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kuwasaka pamoja na kutafuta silaha zetu lakini hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa … zipo simulizi mbalimbali zinazoendelezwa kwenye mitandao ya kijamii ila sisi serikali ya mkoa bado hatujathibitisha kwamba watu hao ni wa kikundi gani ila ninachokifahamu hao watu ni wahalifu”, alisisitiza.
 
Kuhusu kuongezeka kwa matukio  katika maeneo mbalimbali mkoani humo,  alisema kila tukio linachukuliwa kwa uzito mkubwa na linashughulikiwa kwa namna linavyotokea.
 
Aidha, amewataka wakazi wa Tanga hususan wanaoishi eneo la Amboni na vitongoji vyake kuhakikisha wanaendelea kutoa habari sahihi kuhusu watu mbalimbali wanaowatilia shaka . Alisema taarifa hizo zina umuhimu wa kipekee kwa askari katika kufanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao.
 
Kutokana na maswali mengi ya wanahabari na wananchi, kudai kutoridhishwa na mwenendo  wa utoaji taarifa kuhusu tukio hilo, Mkuu wa Mkoa aliruhusu watembelee eneo la tukio  kuthibitisha kama hali ni shwari katika eneo husika.
 
Timu ya wanahabri takribani 10 kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakiwa chini ya ulinzi wa askari walipelekwa eneo la tukio, ambalo liko umbali wa takribani kilometa tano kutoka yaliko Mapango ya kihistoria ya Amboni.
 
Eneo hilo limetawaliwa na miamba ya mawe makubwa yenye mapango, ambayo hayatumiki kwa shughuli za kihistoria, kama ilivyo katika kitongoji cha Kiomoni yalipo mapango ya kihistoria ya Amboni.
 
Shughuli zinazoonekana kufanyika jirani na eneo hilo, ni ulipuaji wa miamba kwa kutumia baruti ambao hufanywa na wachimbaji wadogo kisha kuvunja kokoto  kwa ajili ya viwanda vya kutengeneza chokaa pamoja na mawe kwa shughuli za ujenzi mjini hapa.
 
Eneo wanakodaiwa kuishi wahalifu hao,  liko umbali wa meta 300 kutoka upande wa pili zinapofanyika shughuli za upasuaji  kokoto zinazoendeshwa na wakazi wa kitongoji cha Majimoto na Mafuriko huko Amboni.
 
Katika eneo hilo,  kulikuwa na ukimya kutokana na kutokuwapo shughuli yoyote hususani uvunjaji kokoto iliyozoeleka kutokana na wananchi kusimamishwa kutokana na tukio hilo.
 
Waandishi wa habari walilazimika kufuata maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na wanausalama waliokuwa wakiwaongoza  kufika ndani ya pango husika.
 
Mwonekano wa eneo hilo, ulidhihirisha ni la hatari kutokana na mapango kufunikwa na vichaka. Ndani ya pango hilo, upo uwazi mkubwa unaoashiria uwepo wa shughuli za kibinadamu zilizokuwa zikiendelea.
 
Ndani ya pango hilo, zilikutwa nguo; hususan suruali, madumu ya kuhifadhia maji, vikombe kadhaa vya plastiki, chupa za maji ya kunywa zilizotumika hatua ambayo imedhihirisha kuwapo binadamu waliokuwa wakikaa humo licha ya kwamba, kufika kwake ni kwa shida.
 
Wakazi wazungumza
Wakizungumza na waandishi, baadhi ya wakazi wa maeneo jirani na eneo hilo, walisema hawajaruhusiwa kufika eneo hilo kwa kuwa linaendelea kulindwa  na askari wa Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU)  kwa kushirikiana na JWTZ.
 
“Muda mfupi tu kabla ya ninyi kwenda huko, askari wa FFU walitoka huko , ninyi mnaelezwa kwamba pako shwari lakini sisi bado hatujaruhusiwa kufika kule kwa sababu panalindwa muda wote na askari… ,” alisema mkazi  aliyejitambulisha kwa jina moja la Mrisho.
 
Katika hatua nyingine, askari wa JWTZ aliyefariki wakati akitibiwa kwenye Hospitali ya Bombo baada ya kujeruhiwa kwenye mapigano hayo ya mwishoni mwa wiki,  mwili wake uliagwa jana mjini hapa kabla ya kusafirishwa kuelekea wilayani Korogwe kwa maziko yaliyofanyika katika kijiji cha Bungu.

Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta Amsimamisha Kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),Madeni Kipande 


Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande kutokana na kile kilichoelezwa kuwa uendeshaji mbovu wa utoaji wa zabuni.

Aidha, amemteua Awadhi Massawe kushika wadhifa huo. Kabla ya uteuzi huo, Massawe alikuwa Meneja wa Bandari.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, Sitta alisema uamuzi huo umetokana na kuwapo malalamiko ya kutofuatwa kwa taratibu za zabuni na ucheleweshaji wa barua kwa wanaoshinda.
 
“Ni muhimu sana taratibu zetu za ununuzi katika bandari ziwe wazi na ziheshimike duniani kote, maana miradi hii ni mikubwa sana inayopitishwa na bodi ya zabuni ya TPA,” alisema.
 
Sitta alisema,  aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Dk Harrison Mwakyembe alianza kushughulikia masuala hayo, lakini hayajakaa vizuri. Alisema hakuna uwazi na kumekuwa na ubabaishaji mkubwa, ikiwemo kubadilika majina ya kamati za kutathmini zabuni.
 
Wakati huo huo  Sitta ameunda timu ya watu sita itakayochunguza tuhuma za Kipande. Imepewa wiki mbili iwe imefanya kazi hiyo.
 
Timu hiyo itaongozwa na Jaji mstaafu, Augusta Bubeshi na Katibu wake, Deogratius Kasinda ambaye ni mtumishi wa Wizara ya Uchukuzi.
 
Wajumbe wengine wa timu hiyo ni Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Manunuzi ( PPRA) Dk Ramadhani Mlinga, Samson Lugigo , Happiness Senkoro na Flavian Kinunda ambao walishawahi kushika nyadhifa za juu ndani ya TPA.
 
“Nimejitahidi kuchukua hawa wastaafu kwa sasa hivi hawatafuti cheo chochote, naamini watatenda haki, watachunguza tu bila kufanya uonevu,” alisema Sitta.
 
Waziri Sitta alisema bandari ni eneo muhimu, kwani takwimu zinaonesha kwamba asilimia 43 ya makusanyo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), yanatokana na kodi ya ushuru wa forodha. Kati ya makusanyo hayo, asilimia 87 yanakusanywa kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
 
Kwa upande wa Kipande,  alisema hawezi kupinga hatua iliyochukuliwa na waziri .
 
Hata hivyo, alisema anaamini kipindi chote cha uongozi wake, alifanya ambayo yalikuwa sahihi na hana wasiwasi na uamuzi huo.
 
"Mimi sina wasiwasi na hilo sababu huo ni uamuzi wake; lakini nina imani kuwa katika bandari hii, nimefanya kile ambacho nilikuwa natakiwa kufanya,  hivyo sina shaka na hilo," alisema Kipande.
 
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto ametaka serikali kujenga matangi ya kuhifadhia mafuta na kujenga bomba la mafuta kwenda mikoani.
 
Aidha, kamati hiyo imetaka TPA kuangalia uwezekano wa kununua hisa 50 za Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta (Tiper) imilikiwe kwa asilimia 100 na Serikali.
 
Kuhusu ujenzi wa matangi, Zitto alisema hatua ya Serikali kujenga matangi yake ya kuhifadhi mafuta, itasaidia kujua kiasi cha mafuta yanayoingia na kuweza kukadiria kodi kwa uhakika.
 
Akitoa mfano wa Kenya, alisema Serikali inamiliki matangi ya kuhifadhia mafuta,  wanayapima kujua kiasi cha mafuta kilichoingia na kukitoza kodi  kabla ya kupelekwa kwenye matangi ya waagizaji.
 
“ Walichofanya, wamemtaka kila muagizaji kuwa na flow meter  yake na yakitoka kwenye meli yanaingia kwenye matangi ya Serikali na baada ya kujua kiasi na kutozwa kodi hupelekwa kwa walionunua,” alisema.
 
Zitto  alisema wakati umefika sasa kwa serikali kujenga mabomba ya kusafirishia mafuta na kwa kuanzia yakawa matatu, ambayo yatasaidia kuondoa mfumo wa sasa wa kusafirisha kwa magari.
 
“Linaweza kujengwa bomba moja kwenda Mbeya, likawa na matoleo kwa ajili ya mikoa ya Morogoro, Iringa na mikoa iliyo jirani, kwa kufanya hivyo tutaondoka na hali ya sasa ya kusafirisha mafuta kwa magari,” alisema.
 
Alisema katika kuimarisha reli, ni vyema ukaanzishwa mfumo wa kutoza kodi asilimia 1.5 kwa kila bidhaa inayoingia nchini na fedha hizo ziimarishe usafiri wa reli.
 
“Kwa sasa asilimia 99 ya mizigo inasafirishwa kwa barabara, hili si jambo jema kwa uchumi, najua nikisema hivyo wenye malori watalalamika, lakini wanaweza kufanya biashara nyingine,” alisema.
 
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TPA, Awadhi Massawe alisema asilimia 60 ya mafuta yanayoingia nchini hupitia kwenye boya la Single Buoy Mooring (SBM).
 
Alisema wamejipanga kujenga mita ya kisasa ya kupimia mafuta maeneo ya Kigamboni huku ile ambayo haitumiki, wamepanga kuiboresha na kuwa ya kisasa.
 
Kuhusu maendeleo ya ujenzi wa gati namba 13 na 14 ambazo zabuni  yake iliingia utata, Massawe alisema ripoti ya maandishi wataipeleka kwa Kamati hiyo ya Bunge ifikapo Machi Mosi mwaka huu.
 
Pia, Massawe alisema hatua ya kitengo cha kupakua kontena kupewa mtu binafsi, inawapunguzia mapato na kuwa hiyo ndio sekta ambayo inaingiza fedha nyingi.
 
Alisema ili kupambana na hali hiyo, wamejipanga kuimarisha gati namba 1 hadi 7 na kuongeza kina cha bahari ili kuweza kupakua makasha na kuwa kwa mwaka jana waliweza kupakua makasha laki mbili

Ajira 40,735 Zazalishwa Ndani ya Miezi Mitatu 


Ajira 40,735 zimezalishwa ndani ya miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka jana na kufanya jumla ya ajira 173,787 kupatikana kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana.

Wizara ya Kazi na Ajira imesema ongezeko hilo la ajira limejitokeza katika maeneo makuu mawili ikiwemo ajira serikalini ambazo ni 2,652 sawa na asilimia 6.5 na ajira kupitia sekta rasmi binafsi ambazo ni 38,083 sawa na asilimia 93.5.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Wizara hiyo, Ridhiwan Wema alisema takwimu hizo zinaonesha kwamba sekta binafsi imeendelea kuwa mhimili wa uzalishaji wa ajira nchini kutokana na serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya waajiri kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania.
 
“Katika kipindi cha nusu mwaka  sekta binafsi rasmi ambayo ndiyo mwajiri mkuu ilizalisha ajira 173,787 kupitia uwekezaji binafsi ambapo uwekezaji kupitia ujenzi zilizalishwa ajira 107,527, uwekezaji kupitia  Kituo cha Uwekezaji (TIC) ajira 34,184 na Sekta ya Mawasiliano ajira 342” alisema.
 
Alisema hatua zinazochukuliwa kwa sasa ni pamoja na kufanya marekebisho ya Sera ya Ajira ya 2008, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Namba 6,2004, Sheria ya Taasisi za Kazi namba 7,2004 pamoja na kutunga sheria Mpya ya Ajira za Wageni ambayo imelenga kulinda ajira za Watanzania, kuboresha mazingira ya biashara na kuhamasisha uwekezaji.
 
Alishukuru wadau mbalimbali kwa ushirikiano wao kwa kutoa taarifa za ajira kwa wakati. Alitoa mwito kwa waajiri wote nchini kutoa ushirikiano katika ukusanyaji taarifa za soko la ajira.
 
“Taarifa hizi zimelenga kuiwezesha serikali kujua hali ya ajira nchini na kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuwezesha serikali kupanga matumizi sahihi ya nguvu kazi nchini,” alisema.
 
Alisema taarifa hizo ni miongoni mwa vigezo vikuu vinavyotoa picha halisi ya mafanikio ya kiuchumi na kimaendeleo kwa nchi au mahali husika na zinasaidia kupanga, kutekeleza na kupima ufanisi wa mipango ya kiuchumi nchini pamoja na kupima uwezo wa kiuchumi katika wakati husika.