Wabunge walipoingilia kati Wasichana wanaovaa nguo fupi kuchaniwa mavazi hadharani.
Kutoka Kenya kikubwa kilichotawala mitandao na vyombo vya habari kwa mfululizo tangu wiki iliyopita ni kuhusu tukio la wanaume kuwachania nguo hadharani wanawake ambao wanawatuhumu kuvaa vibaya, leo katika taarifa ya habari kituo cha Citizen TV imeripotiwa taarifa kuhusu mwendelezo wa habari inayohusiana na tukio hilo.
Wabunge wamekuwa watu ambao mara nyingi
tumezoea kuwaona wakitetea maslahi ya watu wanaowaongoza, leo kwenye
taarifa ya kituo hicho Wabunge wanawake Kenya pamoja na wanawake wengine
wameandamana kulaani kitendo kinachofanywa na wanaume hao kuwachania
nguo wasichana.
“…Sisi
kama jamii lazima tuwe tunatetea haki za akina mama, au haki za kila
mmoja, uwe mwanaume uwe mwanamke.. Kitendo cha kumvua mwanamke nguo
sijui niseme ni hujuma au niseme vipi.. Kwa sababu kama tutaendelea kuwa
hivyo tutakuwa kama India, India walianza hivyo hivyo.. Kisha wakaanza
‘kuwa-rape’ akina mama..“
“… Kati ya
wanawake watatu at least mmoja amedhulumiwa na mwanaume lakini
hawazungumzi, na hata wakizungumza wanafikiri hawatasikilizwa.. Kwa
hivyo leo hii niko hapa kuwaambia hao wanaume kwamba mtashikwa na
mtachukuliwa hatua…“
Kwa upande wa wanaume ambao wanawafanyia vitendo hivyo wasichana wamesema haya; “…
Tunapinga nguo fupi maana yake kinyume.. Maadili ya Waafrika ni kwamba
avae kinadhifu.. Halafu dini zote hakuna dini inayokubali mwanamke avae
nguo fupi ama mini-skirt fupi…“
Kampeni ya kulaani kitendo hicho imepewa jina la My Dress My Choice.
Hizi ni baadhi ya picha zilizowekwa na Standard Digital zikionyesha maandamano hayo.
No comments:
Post a Comment