Hivi ndivyo alivyouawa nahodha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, azikwa kishujaa
 Mazishi ya aliyekuwa nahodha wa Afrika Kusini Senzo Robert Meyiwa yamefanyika Jumamosi Novemba 1 baada ya kuuawa na majambazi waliovamia nyumbani kwa mchumba wake, Kelly Khumalo .

Mwenyekiti wa klabu Ya Orlando Pirates, Irvin Khoza akitoa heshima za mwisho kwenye mazishi ya Senzo.
Taarifa ya namna mauaji hayo 
yalivyotokea imetolewa, ambapo imesemekana Senzo alikuwa akijiandaa 
kutoka kwenye nyumba ya mama mzazi wa Kelly Khumalo wakati majambazi 
watatu walipovamia nyumba hiyo wakiwa na bastola, wakiwaamuru waliomo 
ndani ya nyumba hiyo kutoa vitu vya thamani walivyonavyo ikiwemo simu za
 mkononi na fedha.
Senzo alikuwa akicheza na mtoto wake 
ndani ya chumba, alitoka kuja sebuleni baada ya kusikia kelele za 
majambazi hao wakati mpenzi wa Senzo alikimbilia chumbani nakujifungia.
Jambazi mmoja alifyatua risasi chini baada ya kushindwa kuufungua mlango alimojifungia Kelly.
Senzo akiwa kwenye harakati za kutoka 
nje ya mlango kufukuzana na jambazi mwingine alipigwa risasi mgongoni 
iliyopelekea mauti yake.


No comments:
Post a Comment