Mapya kuhusu huduma za chakula Mgahawa wa Bunge
“…Naomba
 mwongozo wako kwamba kinachoendelea katika viwanja hivi vya Bunge pale 
Kantini,  kuna mabadiliko makubwa sana yamefanyika kwa watoa huduma 
kiasi kwamba kwanza hata huduma zao na kauli zao kwa wateja wao sisi 
wabunge sio nzuri..“, Hiyo ilikuwa kauli ya mwongozo wa Mbunge 
Martha Mlacha alipopewa nafasi kutoa mwongozo wake katika kikao cha 
Bunge leo Dodoma.
“…Lakini 
kitu ambacho.. ninachokuomba mwongozo  kwamba Bunge hili.. hapa mahali 
hapa.. ndiyo chimbuko na kisima cha watetea haki za Watanzania wote, 
wakiwemo vibarua, wafanyakazi na watu wengine na kwamba kama kuna 
kampuni inachukua ama kufanya biashara kwenye eneo fulani ikakuta 
wafanyakazi maeneo yale, inabidi wafanyakazi wa eneo lile wachukuliwe na
 kampuni ile inayokuja pale…”– Mlata.
“…Kumetokea
 sintofahamu naomba mwongozo wako, hivi sasa vijana thelathini waliokuwa
 wanafanya kazi katika kwenye kantini ile wanarandaranda mitaani 
wanakutana na sisi wabunge wakituomba tuwasaidie hata hela ya kula, 
naomba mwongozo wako ni nini kimetokea?..”– Mlata.
Akijibu mwongozo huo Naibu Spika; “…
 Hili ambalo ameliongea Mheshimiwa Mlatha ni jambo la ndani.. ni jambo 
la kwetu sisi wenyewe, niwahakikishieni waheshimiwa Wabunge kwa kifupi 
sana kwamba jambo hili liko mikono salama ya tume ya huduma za Bunge, 
mabadiliko hayo ni kwa nia njema watumishi waliokuwa pale wengi wao 
wamekuwa deployed tayari maeneo mengine ya kazi..“– Ndugai.
“…Nawapa 
majibu ya uhakika, zaidi ya robo tatu wameshakuwa deployed tayari na 
tulikuwa na kamati ya tume jana wala sio juzi na tumelizungumzia jambo 
hili , wako vijana wachache ambao bado hawajachukuliwa, na hao wachache 
watachukuliwa watapangwa katika maeneo mengine ya shughuli. Kwa hiyo 
liko mikono salama kabisa…“– Ndugai.

No comments:
Post a Comment