TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, November 17, 2014

Labda hautopenda hizi picha za harusi ya Solange zikupite…. kuhusu Jay Z kuhudhuria je?

Solange Knowles Marries Alan Ferguson - Rehearsal Dinner 
Siku ya Novemba 16 kulikuwa na taarifa kuhusu sherehe ya kuagwa kwa Solange Knowles ambapo shemeji yake ambaye ni Jay Z hakuhudhuria sherehe hiyo, leo kuna story kuhusu ndoa yake, unadhani Jay Z hakuhudhuria tena?
Wengi wamekua na shauku ya kujua kama alihudhuria na hii ni kutokana na Jay Z kuonekana akipigwa na Solange kwenye lift miezi kadhaa iliyopita, sasa taarifa ikufikie tu kwamba Jay Z alikuwa mmoja kati ya wageni waalikwa ambao jumla walikuwa mia mbili kwenye hiyo sherehe ya ndoa ya Solange jana Novemba 16 2014 na  Beyonce nae akiwemo.
Huenda ndoa ya Solange na Alan Ferguson iliyofungwa katika kanisa la Holy Trinity, New Orleans imekuwa ya siri kama ilivyokuwa ya Jay Z na Beyonce kwa kuwa mpaka sasa hakuna picha zilizoenea mitandaoni zikionyesha ikifungwa.
Alan ni director wa video za muziki ambapo alishawahi kufanya video za Beyonce na Jay Z kwa nyakati tofauti siku za nyuma.
Tumezoea kuona maharusi wakibebwa kwenye magari ya kifahari kwenye harusi zao ila hii ya Solange ilikuwa tofauti kama unavyoona kwenye picha ambapo ilikua siku ya Jumamosi Novemba 15 wakati wa sherehe ya utangulizi siku moja kabla ya ndoa yao ambapo Jay Z hakuonekana kwenye hii na headlines ndio zikaanzia hapo.
solange-3-435
solange-alan-ferguson-ride-bikes-to-wedding-pcn-1__oPt
solange-alan-ferguson-ride-bikes-to-wedding-pcn-4__oPt
solange-alan-ferguson-ride-bikes-to-wedding-pcn-5__oPt
solange-alan-ferguson-ride-bikes-to-wedding-pcn-8__oPt

No comments:

Post a Comment