Rais Obama athibitisha kifo cha Kassig
Rais
Barack Obama amethibitisha kifo cha mfanyakazi wa shirika la kutoa
misaada la Marekani Abdul-Rahman Kassig, ambaye ameuawa kwa kukatwa
kichwa na kuonyeshwa katika video iliyorushwa na kundi la Islamic State
(IS).
Bwana
Obama amekitaja kitendo hicho kuwa "uovu uliopitiliza" na kutoa salaam
zake za rambirambi kwa familia ya Bwana Kassig, aliyekuwa na umri wa
miaka 26, ambaye alitekwa nyara nchini Syria mwaka jana.
Video
hiyo ambayo imethibitishwa na Ikulu ya Marekani, inamwonyesha mtu
aliyejificha uso akiwa amesimama juu ya kichwa cha Bwana Kassig.
Abdul-Rahman(Peter) Kassig akionyeshwa katika picha akigawa chakula kwa wakimbizi nchini Lebanon Mei 2013
Pia inaonyesha kukatwa vichwa kwa raia 18 wa Syria waliotambuliwa kama maafisa wa jeshi na marubani.
Rais
Obama amempongeza Bwana Kassig kama mtu wa kutoa msaada kwa watu wengine
na kusema " alichukuliwa kwetu katika kitendo cha uovu wa kupitiliza
uliofanywa na kikundi cha kigaidi ambacho ulimwengu unakihusisha na
unyama".
"leo
tunatoa sala zetu na rambirambi kwa wazazi na familia ya Abdul-Rahman
Kassig, ambaye pia tulimjua kwa jina la Peter," amesema.
Kauli ya
Bwana Obama imekuja wakati akirejea Marekani kutoka Australia ambako
alikuwa akihudhuria kikao cha viongozi wa nchi za G20.
Kikundi cha IS, ambacho kinadhibiti sehemu kubwa ya Syria na Iraq, mpaka sasa kimewaua mateka watano kutoka nchi za magharibi.
Wengine ni Waingereza Alan Henning na David Haines, na waandishi wa habari wa Marekani James Foley na Steven Sotloff.
Mauaji
hayo yalitekelezwa na mtu anayeaminika kuwa Mwingereza. Ndevu za mtu
huyo zinafanana na wapiganaji walioficha nyuso zao wakiwa wamepigwa
picha ya video wakimwonyesha Bwana Kassig.
Tofauti
na video zilizotolewa siku za nyuma na kundi la IS, video hii mpya
inaonyesha sura za wapiganaji wengi wa jihad na wanaonyesha sehemu yake
kuwa ni Dabiq katika jimbo la Aleppo nchini Syria.
Bwana Kassig alikuwa askari wa zamani wa Marekani ambaye alitumikia jeshi la nchi hiyo nchini Iraq.
Baadaye
alifundishwa kama mtaalam wa matibabu ya dharura na kuanzisha shirika la
kukabiliana na matukio ya dharura na msaada (Sera), likisaidia
kusambaza misaada katika makambi yaliyo katika pande zote mbili za mpaka
wa Syria.
Alikuwa
akiandaa mradi kwa ajili ya shirika lake la Sera alipotekwa mwezi Oktoba
2013 wakati akisafiri kuelekea mashariki mwa Syria.
No comments:
Post a Comment