Baada ya Shy-Rose Bhanji kudaiwa kumpiga mbunge mwenzake, hiki kimesemwa bungeni
Kumekuwa
 na taarifa kuhusu kuwepo migogoro mbalimbali inayohusisha Wabunge 
wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki ambapo Mbunge 
Shy-Rose Bhanji amehusishwa sana kwenye vichwa vya habari.
Kwenye kikao cha Bunge November 20 2014 Dodoma Hatibu ambae ni mbunge wa Zanzibar aliuliza >>> “…
 Sisi wabunge wa bunge hili ndiyo wapiga kura wa kuwachagua wawakilishi 
wetu wa kutuwakilisha katika bunge la Afrika Mashariki, kumekuwa na 
taarifa za kulipaka Taifa hili matope kulitia aibu kutokana na  baadhi 
ya wawakilishi wetu, Wabunge wetu wa Afrika Mashariki kutokana na 
matendo wanayoyafanya kule..”
“…Ni
 lini hasa kinachoendelea pale na hatua gani zilizochukuliwa kuhusu 
ukosefu wa nidhamu uliojitokeza kwa mbunge Shyrose Banji wazi wazi na 
bili hali hakuna taarifa yoyote, Mheshimiwa Naibu Spika naomba mwongozo 
wako…”– Hatibu.
Baada ya swali waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akawasha kipaza sauti na kutoa haya majibu “…Naomba
 nitoe taarifa kwamba kinachotokea katika Bunge la Afrika Mashariki kwa 
kiasi kikubwa kinahusu mgogoro wa  spika mwenyewe, hilo ndiyo chanzo cha
 matatizo mengi, kwa hiyo  wabunge  wa Bunge la  Afrika Mashariki 
wamegawika kataka makundi mawili, kuna kundi linalotaka Spika lazma 
aondolewe, na wengine wanadai wanamtetea abaki…”
..Sasa katika kundi ambalo wanataka abaki imeonekana Tanzania ndio kikwazo, kwa sababu ili upate uamuzi ndani la Bunge la Afrika Mashariki katika suala lolote lazima upate akidi inayotosheleza kutoka kila nchi, sasa wabunge wa Tanzania ambao mwanzoni waliunga mkono hoja ya kumuondoa yule Spika wamefuta hilo na wamekubaliana aendelee kwa hiyo imeleta chuku kiasi Fulani…“– Sitta.
 “…Katika 
tukio ambalo limetokea juzi na nasema hivi kwa sababu  Naibu Waziri 
wangu yuko kule kwa hiyo ni jambo halisi, kilichotokea sio kama 
kinavyoelezwa Mheshimiwa Shyrose Banji ambaye anahesabika ni mfuasi 
mkubwa wa Yule Spika kiasi kwamba wenzie wanamuona kama kibaraka vile, 
alikuwa anapita katikati ya Wabunge wengine kuwahi usafiri kwa bahati 
mbaya akamgonga Mheshimiwa Ndelakindo Kessy, Mheshimiwa Ndelakindo 
akahamaki na kwa kusaidiwa na  baadhi ya Wabunge  wengine wa Uganda 
akaenda kituo cha Polisi kutoa taarifa kwa madai kwamba amefanyiwa 
makosa ya jinai wanaita ‘assaults’…“– Sitta.
“
“>…Ikabidi aitwe ‘Sergeant at Arms’ wa Bunge la EALA ambaye 
alikwishaanza jitihada za kulifanya jambo lile liishie ndani ya Bunge na
 katika jitihada hizo alifika mbali kidogo akawezesha Wabunge wetu hao 
wawili waweze kusikilizana na ninavyotoa taarifa hivi sasa ni kwamba 
jana suala hili limekwisha na haliendelezwi na Polisi tena…
“– Sitta.
Hivi ndivyo Waziri Sitta alimalizia kujibu suala hilo; “…Sasa
 yale mengine yaliyosema kwamba alifanya mambo ya hovyo Mheshimiwa yule 
tena kama miezi miwili iliyopita, bado yako mikononi mwa tume ya Bunge 
la Afrika Mashariki hadi hapo watakapolishughulikia hatuwezi kufanya 
kitu chochote, na tukishapata taarifa ya tume ya Bunge la Afrika 
Mashariki basi mimi nitatoa taarifa kwa Mheshimiwa Spika ili sasa sisi 
kwa wote kama jimbo la uchaguzi La Wabunge hao tuone ukweli ni upi na 
tujue hatua ya kuchukua..”– Sitta.

No comments:
Post a Comment