AFCON 2015 VS Ebola hatma kujulikana leo
Shirikisho la soka barani Afrika CAF hii leo linatarajiwa kukaa kikao chake cha mwisho kitakachofikia maamuzi ya kufanyika ama kutofanyika kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015.
Kikao hicho kitahusisha uongozi wa CAF , kamati ya maandalizi pamoja na uongozi wa juu wa serikali ya Morocco kufikia uamuzi wa mwisho wa kusogeza mbele michuano hiyo au kuruhusu ifanyike kama ilivyopangwa .
Michuano hiyo iliyopangwa kufanyika mwezi januari mwaka 2015 kama ilivyo kila baada ya miaka miwili imeingia kwenye hati hati ya kufanyika kufuatia hofu ya ugonjwa wa ebola ambayo imesababisha wenyeji Morocco kuomba michuano hiyo kuahirishwa .
CAF ilianza mchakato wa kutafuta mwenyeji mbadala ambapo ilizungumza na mataifa kama Afrika Kusini , Ghana na Misri kuwaandaa kama Morocco wataendelea na msimamo wao wa ktuaka michuano hiyo kuahirishwa au kuhamishwa na Ghana pamoja na Misri wameonyesha dhamira ya kuwa wenyeji .
Afrika Kusini kwa upande wao wamejitoa kwenye mchakato huo baada ya waziri wa michezo wa taifa hilo Fikile Mbalula na rais wa chama cha soka SAFA kusema kuwa Afrika Kusini haitakuwa tayari .
Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa kawaida hufanyika kila baada yua miaka miwili na mara zote huwa inafanyika mwezi januari lakini kwa michuano ya mwaka 2015 hali inaweza kuwa tofauti kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola ambao hadi sasa umesababisha vifo vya watu zaidi ya 3000 huku mataifa ya Afrika Magharibi yakiathirika zaidi
No comments:
Post a Comment