TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, November 11, 2014

Mambo mapya 7 aliyoyazungumza Dr. Mwakyembe bungeni kuhusu Treni Tanzania

Screen Shot 2014-11-12 at 1.19.18 AM
Hii picha sio Mabehewa yanayozungumziwa.
Waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe ni miongoni mwa viongozi wa Tanzania ambao wakisimama sehemu yoyote kuzungumza lazima mwandishi yeyote ataiweka kalamu yake vizuri kujua lazima mazito ya kuwafikishia Wananchi yawepo.
Kwenye bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania November 11 2014 Dr. Mwakyembe amezungumzia ishu 7 kuhusu usafirishaji kwa njia ya reli Tanzania.
1 ‘Tumewezeshwa na serikali kuunda upya vichwa vinane vya Treni kwenye karakana yetu ya Morogoro, ndio unaona sasa hivi Treni zikipita vinafanya kazi, tumeingiza vichwa vingine nane karakana ya Morogoro vitatoka mwezi wa tano’
Screen Shot 2014-11-12 at 1.54.32 AM 
2 Benki ya dunia sasa hivi tunaanza mchakato tunapata vichwa vitatu vipya pamoja na Mabehewa 44 kuanzia Dar es salaam kwenda Isaka, Mamlaka ya bandari baada ya kuona benki ya dunia inaleta vichwa vitatu nayo imetafuta vichwa vitano vya treni navyo vinaingia karakana ya Morogoro.
3 Tumenunua Mabehewa mapya ya mizigo 274 tunaanza kuyapepea mwezi huu bandari ya Dar es salaam, ni bunge hilihili ambalo limeniruhusu ndani ya mwaka huu wa fedha tuagize Mabehewa mengine ya mizigo 204.
4 Tumenunua vichwa vingine vya Treni 13 navipokea January 2015 na vilevile bunge hili limeruhusu tununue vichwa vingine 11 ndani ya mwaka huu wa fedha.
Screen Shot 2014-11-12 at 1.50.34 AM 
5 Tumenunua Mabehewa 22 mapya ya abiria, nataka tu kutoa agizo kwa Mamlaka ya reli kwamba tutakapopata Mabehewa 22 ya abiria January 2015, ratiba ibadilike sasa tuwe na safari tatu kwa wiki za Treni ya abiria kuanzia Dar es salaam kwenda bara na kutoka bara kuja Dar es salaam na mwezi wa nne tutakua na Treni ya abiria mara nne kwa wiki.
6 Reli yetu ni ya zamani sana ina umri wa zaidi ya miaka 100 mnajua, inahitaji matengenezo makubwa na wengi wanasema si mngeing’oa tu hiyo muweke reli mpya? sawa lakini kuing’oa reli iliyopo na kujenga nyingine mpya hautakuwa uamuzi mzuri sana manake tutakwamisha uchumi wa nchi yetu.
7 Ni kweli tunajenga reli nyingine ya pili na tuko kwenye harakati za kutafuta pesa na itajengwa kwenye kordo hiyohiyo ya reli kuanzia Dar es salaam kwenda Kigoma, Mwanza, Mpanda na sasa tunaongeza mpaka Kalema…. huu ni mradi mkubwa sana na utagharimu nchi zaidi ya dola za kimarekani Bilioni 7.6

No comments:

Post a Comment