Jeshi la Kenya kuwasaka wauaji Mandera mpakani mwa Somalia
Bus lililotekwa na wapiganaji wa Al shabab kabla ya kuwaua abiria 28 wasiokuwa waislamu,Mandera mpakani mwa Somalia
Na Martha Saranga Amini
Mshauri
wa juu wa raisi Uhuru Kenyata Abdikadir Mohammed ametoa wito kwa wakenya
wote wa imani zote kuungana pamoja dhidi ya wahalifu.
Hatua
hiyo inakuja kufuatia mauaji ya alfajiri ya jana kutekelezwa na
wapiganaji wa kiislamu kutoka somalia ambao waliteka basi moja na kuwaua
abiria ambao hawakuwa waislamu.(P.T)
Tayari
maafisa wa jeshi la Kenya KDF wamewasili Mandera eneo la mpakani mwa
somalia kuwasaka waliotekeleza mauaji hayo na kuhakikisha ulinzi baada
ya abiria 28 kuuawa mapema jana.
Kundi la
Al-Shabab limesema shambulizi hilo lililenga kulipa kisasi kufuatia
mauaji ya waislamu ambayo kundi hilo limedai kutekelezwa na majeshi ya
kenya katika mji wa pwani wa Mombasa.
Serikali ya kenya imesema imeanza kuwatambua wahalifu hao na itahakikisha inafikisha mbele ya sheria.
Waziri wa
mambo ya ndani Joseph Olellenku amesema kuwa kambi iliyokuwa
inamilikiwa na wapiganaji hao huko mandera imeshambuliwa na jeshi la
kenya.
Chanzo:RFI
No comments:
Post a Comment