TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, November 10, 2014

Kilichoandikwa na Ikulu ya Tanzania baada ya Rais Kikwete kutibiwa Marekani.

Rais Kikwete akizungumza na daktari bingwa wa Upasuaji, Edward Shaeffer.
Siku tatu baada ya kutolewa taarifa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania kuhusiana na safari ya rais Dkt. Kikwete kwenda Marekani kwa ajili ya kupatiwa matibabu, ipo taarifa nyingine kuhusiana na President baada ya kutibiwa.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji wa tezi dume baada ya uchunguzi wa kidaktari kugundua ana tatizo hilo katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland Marekani.
Upasuaji huo umechukua saa moja na nusu na umefanyika salama na kwa mafanikio ambapo sasa hali ya Rais Kikwete inaendelea vizuri japo bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Saa chache zilizopita kupitia ukurasa wa Twitter wa Rais Kikwete (@jmkikwete) Ikulu wameandika >>> “08/11/2014 Mheshimiwa Rais Dkt Jakaya Kikwete alifanyiwa upasuaji wa Tezi Dume uliokamilika salama katika Hospitali ya John Hopkins. – Ikulu
Rais Kikwete akizungumza daktari bingwa wa Upasuaji, Edward Shaeffer na daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi muda mfupi baada ya kuwasili Marekani.
Rais Kikwete akizungumza daktari bingwa wa Upasuaji, Edward Shaeffer na daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi muda mfupi baada ya kuwasili Marekani. (picha zote kutoka Issamichuzi.blogspot.com
Tweet nyingine kwenye Twitter ya President ikasema >>> “Leo 09/11 Mheshimiwa Rais anaendelea vizuri na ameanza mazoezi, tutaendelea kuwajulisha maendeleo yake na tuungane katika kumuombea. – Ikulu
Rais Kikwete akizungumza na daktari bingwa wa Upasuaji, Edward Shaeffer.
Rais Kikwete akizungumza na daktari bingwa wa Upasuaji, Edward Shaeffer.
Rais Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania Marekani, Liberata Mulamula Hospitalini alikolazwa akipatiwa matibabu Marekani.
Rais Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania Marekani, Liberata Mulamula Hospitalini alikolazwa akipatiwa matibabu Marekani.

No comments:

Post a Comment