Umesikia taarifa ya ajali mbaya iliyotokea Mahakamani?

Mtoto wa mwanamke mmoja amefariki wakati
 mama yake alikuwa anapandishwa kizimbani baada ya kukamatwa akiuza 
bidhaa barabarani kinyume na Sheria.
Mtoto mwenye umri wa miaka miwili 
amegongwa na gari na kufa katika Makao Makuu ya Halmashauri ya jiji la 
Kampala KCCA, ambapo mama yake Madina Namakula alifikishwa Mahakamani 
Kampala, Uganda, kusomewa shitaka lake ambapo wakiwa Mahakamani hapo 
ndipo mtoto huyo alipopata ajali hiyo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema kuwa Polisi wamesababisha kifo cha mtoto huyo.
Mtoto huyo amezikwa leo Kampala, Uganda.
No comments:
Post a Comment