Malalamiko ya kukatwa muda wa hewani kwenye simu kwa huduma ambayo hujaitumia yamefika tena Bungeni
Kumekuwa na malalamiko kwa watumiaji wengi wa simu za mkononi kutokana na kukatwa gharama za huduma ambazo hawajaziomba, ikiwemo kuunganishiwa miito ya simu na nyinginezo.
Kama hukupata nafasi ya kusikiliza Bunge
jana Novemba 25, ilihojiwa kuhusiana na suala hilo ambapo Naibu Waziri
wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia alitolea majibu pamoja na suala
la baadhi ya maeneo kuwa na matatizo ya mtandao.
“… Katika makubaliano kati ya Serikali na kampuni mpya ya simu ya Viatel,
ambayo imekubali kujenga minara na kupeleka mawasiliano katika maeneo
yote ambayo hayana mawasailiano nchini, tumewapa orodha ya Vijiji elfu
nne ambavyo havina mawasiliano kote Nchini au vina mawasiliano ni
hafifu, na tumekubaliana tumewekeana mkataba kwamba maeneo yote hayo
ikiwemo maeneo ya jimbo na Nyag’wale yatapata mawasiliano kabla ya mwezi
Novemba mwaka huu…“– January Makamba.
“...
Kuhusu miito ambayo inaingiziwa kwa wateja bila ridhaa yao, Serikali
inatambua kwamba hili ni tatizo na sisi kama Wizara tumewaandikia barua
na tumezungumza na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ambayo ina wajibu wa
kusimamia jambo hili kuhakikisha kwamba halifanyiki lakini na maslahi ya
watumiaji wa simu yanalindwa, kwa hiyo tutaendelea kulifuatilia
kuhakikisha kwamba Sheria inazingatiwa ili watumiaji wasidhulumiwe…”– January Makamba
No comments:
Post a Comment