MBRAZIL EMERSON KUZIBA PENGO LILILOACHWA NA JAJA YANGA
Geilson Santana Santos ‘Jaja’.
KLABU ya
Yanga inatarajia kumsajili kiungo mkabaji mpya kutoka Brazil Emerson De
Oliveira Neves Rouqe kuziba nafasi hiyo iliyoachwa na
mshambuliaji Geilson Santana Santos ‘Jaja’ aliyekatisha mkataba wake na
klabu hiyo kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia.
Jaja akishangilia bao lake alilofunga kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Yanga na Thika United ya Kenya.
Taarifa
kutoka Mtandao wa klabu hiyo umesema Emerson De Oliveira Neves Rouqe
'24' atawasili nchini Jumanne mchana kwa ajili ya majaribio na endapo
atafuzu moja kwa moja atajiunga na kikosi cha mabingwa hao mara 24 wa
Ligi Kuu Tanzania bara.GPL(P.T)
Kabla ya
kuamua kuja Tanzania, Emerson alikuwa akiichezea timu ya Bonsucesso FC
inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Brazil, msimu uliopita alikuwa
akicheza soka la kulipwa nchini Poland katika timu ya Piotrkow
Trybunalski FC iliyopo Ligi Daraja la pili nchini humo.
Jaja
mfungaji wa mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Azam FC, kwenye
mchezo wa Ngao ya Jamii Septemba 14 alisaini mkataba wa miaka miwili na
Yanga akitokea timu ya Itabaina FC na ameichezea timu hiyo kwa miezi
minne na kufunga mabao matano katika mechi zote alizoichezea timu hiyo
zikiwemo za mashindano na kifariki.
Jaja
aliifungia Yanga bao la kwanza ilipocheza mechi ya kirafiki kujiandaa na
msimu kwenye uwanja wa Gombani Pemba dhidi ya Chipukizi na kisha
alifunga bao lake la pili katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa
uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Thika United
ya Kenya lakini mashabiki na baadhi ya viongozi wa Yanga hawakuwa
wakifuraishwa na kiwango chake.
Mshambuliaji
huyo alionekana kuwapa matumaini mashabiki wa Yanga baada ya kufunga
mabao mawili safi katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya bingwa mtetezi
Azam FC huku bao la pili akilifunga kwa ustadi mkubwa na kuwaziba mdomo
mashabiki waliokuwa wakimdhihaki baada ya hapo mechi za Ligi Kuu
zilianza na ukame wa mabao ukatawala sana kwake ikiwa ni pamoja na
kukosa mkwaju wa penalti katika mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Mtibwa
Sugar kwenye uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro.
Staa huyo
aliibuka tena katika mechi ya nne ya Ligi dhidi ya Stand United ya
Shinyanga kwa kufunga bao lake la kwanza katika ligi na la mwisho baada
ya hapo mashabiki hawakuwa wakifurahia anapopewa nafasi uwanjani na
kocha raia mwenzake wa Brazili, Marcio Maximo.
No comments:
Post a Comment