MEMBE AFUNGUA MKUTANO KUHUSU SAYANSI YA JAMII
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)
akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kuhusu
Sauti ya Kwanza ya Sayansi ya Jamii. Mkutano huo ambao unafanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani chini ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam unawashirikisha Wajumbe kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Ghana,
Nigeria na Canada. Katika hotuba yake Mhe. Membe alisisitiza umuhimu wa
Wasomi na Wanazuoni kujikita katika Tafiti za Kisayansi ili kuja na
majibu yatakayoisaidia nchi kuondokana na umaskini, utunzaji wa
mazingira na masuala mengine ya manufaa kwa nchi.
Mhe. Membe akikaribishwa na Prof. Florence Luoga ambaye ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kuhusu Sauti ya Kwanza ya Sayansi ya Jamii ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mhe. Membe akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mkutano huo.(Martha Magessa)
JUU NA CHINI: Ni sehemu ya Wajumbe wakifuatilia mkutano huo kuhusu masuala ya Sayansi ya Jamii.
<
Mhe. Membe akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi huku wajumbe wakimsikiliza.
Sehemu ya wajumbe wakifurahia jambo wakati Mhe. Membe (hayupo pichani) akitoa hatuba ya ufunguzi.
Mhe.
Membe akisindikizwa kwenda kupiga picha ya pamoja na Maprofesa wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwepo kwenye mkutano huo
Mhe. Membe (wa tatu kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano kuhusu masuala
Waziri Membe akifurahia jambo na mmoja wa Wajumbe wanaoshiriki mkutano huo.
Mhe. Membe akihojiwa na Wanahabari kuhusu mkutano huo. Picha na Reuben Mchome
No comments:
Post a Comment