Kiemba aanza kupiga kazi Azam
Amri Kiemba
AMRI
Kiemba ataanza mazoezi kwenye kikosi chake kipya cha Azam FC leo
Jumatatu, lakini ametoa la moyoni kwa kusema, yaliyomtokea Simba
hayamuumizi kichwa na anayachukulia kama sehemu ya changamoto na sasa
ametua kwa Bakhresa kila kitu amemwachia Mungu ili aamue hatma yake.
Lakini
akaenda mbali na kuwaambia mabosi wake wa sasa, yeye hajui kuchagua,
wampe jezi yenye namba yoyote ile iliyopo au watakayoona inamfaa
ataivaa.
Kiemba amekwenda Azam kwa mkopo na dau la Sh10 milioni akitokea Simba.(P.T)
Mchezaji
huyo ameliambia Mwanaspoti kuwa: "Tukijaaliwa kesho (leo) nitaanza
mazoezi rasmi. Binafsi nimejiandaa vizuri lakini siwezi kutoa ahadi
nyingi kila kitu nimemwachia Mungu aamue."
"Unajua
wakati mwingine binadamu tunakosea, unasema nitafanya hiki na hiki
lakini utambue kuwa yote yanapangwa na Mungu kikubwa naomba
ushirikiano,"alisema Kiemba ambaye amebakiza miezi sita Simba na
amekwenda kwa mkopo Azam kwa miezi sita.
"Unaweza kukuta, hata hicho kilichonitokea Simba, ilipangwa tu ili kifanyike hiki kilichofanyika."
Akizungumzia sakata lake Simba, Kiemba alisema:
"Yote
nayachukulia kawaida tu kuwa ni sehemu ya changamoto za maisha, ndivyo
ilivyokuwa imepangwa, sitaki kuyazungumzia sana kwa undani."
Hadi
kutua kikosini hapo, Kiemba alikuwa amesimamishwa na uongozi wa Simba
kwa kile kinachodaiwa ni utovu wa nidhamu. Alisimamishwa pamoja na
wachezaji wenzake, Shaaban Kisiga 'Marlone' na Haroun Chanongo.
Chanzo:Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment