Mwingine aliyehukumiwa kwa kosa la kuzamisha Meli kwa uzembe
Wiki moja baada ya Nahodha wa Meli iliyozama kuhukumiwa kifungo cha miaka 36, na wenzake 13 hukumu ya miaka 30 kila mmoja, kumbe kuna watu wengine ambao wana hatia kutokana na kupatikana na hatia ya uzembe uliopelekea meli kuzama na kuua watu 300.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
inayomiliki Meli hiyo ya Mv. Sewol, Kim Han-Sik, amehukumiwa kifungo
cha miaka 10 jela baada ya kukutwa na hatia ya kuruhusu meli hiyo
kupakia mizigo kuzidi uwezo wake.
Mbali na mkurugenzi huyo, wengine 9
wamehukumiwa miaka 6 kila mmoja na mmoja kati ya watuhumiwa ameachiwa
huru kwa kukutwa bila hatia.
No comments:
Post a Comment