Baada ya David Moyes kukaa benchi kwa miezi kumi, hii ndiyo timu iliyompa kibarua kingine
Ule msemo wa waswahili usemao “ukiona
cha nini mwenzio anajiuliza atakipata lini” umejidhihirisha kwa kocha
wa zamani wa Manchester United David Moyes ambaye ameteuliwa rasmi kuwa
kocha wa klabu inayoshiriki ligi ya Hispania, Real Sociedad.
Sociedad wamemuajiri Moyes wakimpa
mkataba wa miezi kumi na nane ambayo ni sawa na mwaka mmoja na nusu
ambapo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jagoba Arrasate ambaye
alifukuzwa kazi kufuatia timu hiyo kupata matokeo mabaya katika michezo
yake ya ligi .
David Moyes ambaye amekuwa nje ya mchezo wa soka bila ajira yoyote
kwa miezi 10 tangu alipofukuzwa kazi na timu Manchester United alichukua
takribani wiki moja kabla ya kufikia uamuzi wa kuichukua klabu hiyo
japo alishindwa katika jaribio lake la kumshawishi beki wa zamani wa
Manchester United Phil Neville kuungana naye kama msaidizi wake .Moyes ambaye ni raia wa Scotland anakuwa kocha wa tatu toka visiwa vya Ufalme Wa Uingereza yaani United Kingdom kuwa kocha wa klabu hii ya Real Sociedad waliopita kabla yake wakiwa John Tosha na Chirs Coleman wote wakitokea Wales.
No comments:
Post a Comment