TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, November 11, 2014

Kwa hiyo vipi kuhusu AFCON 2015? msimamo wa Morocco? kina nani wako kwenye mazungumzo?

Screen Shot 2014-11-12 at 12.39.26 AM
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limewaondoa wenyeji Morocco kwenye mashindano ya AFCON baada ya taifa hilo kushikilia msimamo wake wa kutokuwa tayari kuandaa michuano ya AFCON mwaka 2015 kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola.
Morocco ambao walikuwa wamefuzu moja kwa moja kama wenyeji hawataweza kushiriki michuano hiyo na badala yake nafasi waliyokuwa nayo itakwenda kwa timu nyingine ambayo itachukua jukumu la kuandaa michuano hii.
Hizi hapa chini ndio timu ambazo ziko kwenye mazungumzo na CAF kuhusiana na nani kuwa mwenyeji wa AFCON 2015.
Nchi ambazo CAF inafanya nazo mazungumzo kuhusiana na kuwa mwenyeji wa AFCON 2015.
.
Awali CAF ilitoa mpaka Jumamosi iliyopita kwa Morocco kuthibitisha uamuzi wake ambapo taifa hilo lilishikilia uamuzi wake wa kutokuwa tayari kuandaa mashindano haya huku kukiwa na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola.
Hatua inayofuata kwa CAF ni kufanya mazungumzo ya haraka na mataifa kadhaa yaliyoonyesha dhamira ya kuwa wenyeji wa michuano hii ili kuhakikisha inafanyika kama ilivyopangwa hapo awali katika ratiba ya kila mwaka ya CAF.
Mwenyeji mpya wa mashindano haya yatakayoanza January 17 hadi February 8 atatajwa Jumatano Tarehe 12 baada ya kamati kuu ya shirikisho hilo kujiridhisha na uwezo wa moja wapo kati ya mataifa yaliyojitokeza.

No comments:

Post a Comment